TAMKO LA DED NKASI KUWALINDA WANAFUNZI WENYE UALBINO DHIDI YA JUA KALI-Agosti 23.2017

MKURUGENZI wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa Julius Kaondo amewapiga marufuku walimu wa shule za msingi na sekondari kuacha tabia ya kuwafanyisha kazi ngumu na kwenye jua kali wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi albino kwa kuwa kufanya hivyo wanawahatarisha afya zao na kupelekea kupata saratani ya ngozi.

Akizungumza jana wakati akizindua kituo maalumu cha upimaji wa kielimu (Nkomolo Assessment Centre) Kilichopo Katika eneo la shule ya msingi Nkomolo wilayani humo mkurugenzi huyo alisema kuwa kitendo hicho kinahatarisha afya za wanafunzi hao na hivyo kuwaweka Katika mazingira ambayo yanaweza kufupisha maisha yao.
Alisema kuwa watu wenye matatizo ya ualbino hawapaswi kukaa Katika mionzi mikali ya jua kwani Inawasababishi ngozi zao kupata saratani hivyo ni busara kuwachukulia kuwa ni watu maalumu na wanahitaji uangalizi maalumu ilikuwakinga na maradhi ambayo yanaweza kuwadhuru.
Aliwasisitiza wanafunzi wote wenye ualbino kutumia mafuta yao maalumu wanayopewa kama msaada ama kuyanunua ili kuzuia mionzi ya jua kwani baadhi yao wamekuwa hawayatumii kwakukosa elimu sahihi na hivyo kujikuta wakisumbuliwa na matatizo ya ngozi.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa ainatofauti wakati mwingine wao wenyewe wamekuwa hawajijali hata wanaposaidiwa na wahisani mbalimbali inawezekana nikutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ama kujikatia tamaa.
Awali akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo mkurugenzi wa maradi huo unaojulikana kama international aid service ( ias) Irene Shayo alisema kuwa maradi huo unafadhiliwa na nchi ya Denimark wakishirikiana na kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania(FPCT).
Alisema kuwa mpaka hivi sasa kituo kikubwa ni kilichopo wilayani Nkasi ambacho kitatoa majibu ya changamoto nyingi zinazowakabili wakazi wa mikoa hiyo miwili na aliwasisitiza kukitumia iliwanufaike na uwepo wakituo hicho.
Shayo aliwasihi watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na ulemavu wa ainaningine kujijali nakujipenda waowenyewe kwani pamoja na changamoto walizonazo bado wanaweza kufanya mambo makubwa ambayo hata wasiowalemavu wananashindwa hivyo ni kuhakikisha wanapambambana bila kukata tamaa.
Alisema kuwa zipo fursa nyingi hivyo basi wajitahidi kujituma Katika kutafuta fursa hizo kwani kuamini kuwa wao ni walemavu na hawawezi kufanya kila kitu  kunasababisha baadhi yao kubakia Katika lindi la umasikini wakati wanauwezo wa kuyabadili maisha nakujipunguzia changamoto walizonazo kwa kutumia fursa zilizopo.
Wiki mbili zilizopita mkurugenzi wa ias Tanzania Bi.Irene Shayo alikuwa mkoani Katavi akiwa na timu yake kwa ajili ya kugawa mafuta maalumu yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi albino katika hali ya kupambana na mionzi mikali ya jua inayowaathiri.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA