MKOANI KATAVI SIMBA AVAMIA KIJIJI MTOTO ANUSURIKA KUTAFUNWA-Agosti 31,2017



MTOTO mmoja mwenye Umri wa miaka 13 Mkazi wa Isinde kata ya Mtapenda,Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi,amenusurika kufa baada ya kushambuliwa na Simba akiwa nyumbani kwao.
Inaelezwa kuwa smba huyo alivamia kijijini hapo majira ya saa kumi usiku wa jana mpaka alipoanza kumshambulia mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Nyutuliangila Madirisha.

Mganga mkuu wa hospital ya manispaa ya Mpanda Dr Theopister Elisa amethibitisha kumpokea majeruhi huyo akisema anaendelea kupatiwa matibabu zaidi.
Kwa upande wake majeruhi ambaye alikuwa amelala pembezoni mwa zizi la ng’ombe alisema alisikia simba akimpapasa katika mwili wake na ndipo alipompiga simba huyo ngumi na hatimaye simba kumjeruhi katika paja lake la mguu wa kulia mpaka alipopiga kelele na kupewa msaada.
Kwa upande wake baba wa majeruhi mzee Madirisha Lubinza amebainisha kuwa alitoka nje wakati wa saa nne usiku baada ya kusikia kelele wakati huo huo muungurumo wa sauti ya samba ukisikika.
Kwa upande wa diwani wa kata ya mtapendwa Fyula Samwel amesema kuwa simba wapo watatu ambao wanazunguka katika maeneo ya kata hiyo na yameshaua mbuzi 8 na ng’ombe 7 na kumjeruhi mtu mmoja ambapo Mh.Fyula amewataka wananchi kutoenda maeneo ya porini wakiwa mtu mmoja mmoja pamoja na kuacha kutembea wakati wa usiku ili mpaka hali itakapo kuwa nzuri.
Kwa mjibu wa Afisa mtendaji wa kata ya Mtapenda Bw.Joseph Mwamkiri amesema tatizo la Simba lipo kwa muda wa zaidi wiki mbili huku ikisemekana kuwa huenda simba hao wanafuata maji ambapo hata hivyo ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuondoa tatizo hilo kwa sababu linatajwa kutokea zaidi ya mara tatu la simba kuzuru maeneo ya kata ya Mtapenda.
Mwaka uliopita Mzee mmoja akiwa na mjukuu wake katika kata ya Sitalike Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo waliuliwa na Simba huku motto akiliwa mwili wote na samba huyo kubakiza kichwa peke yake.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA