MGOMO WA SIKU 2 WA WAENDSHA BAJAJI MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI WASITISHWAAgosti 9,2017


WAENDESHA pikipiki za tairi tatu maarufu kama bajaji manispaa ya Mpanda Mkoani,wameruhusiwa kusafirisha abiria bila mipaka kwa kupita katika barabara walizokuwa wamezuiliwa ambapo barabara hizo ni pamoja na barabara ya Mpanda-Kigoma,Mpanda Sumbawanga na Mpanda Nsimbo.

Kwa mjibu wa mwenyekiti wa chama cha waendesha bajaji mkoani Katavi Bw.Rashid Juma amesema maamuzi haya yamefikiwa kufuatia maafisa wa usalama wa taifa,Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani,viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM na wadau wengine wa usafiri kukutana jioni hii ili kutafuta mwafaka wa suala hili.
Kwa upande wake Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi kupitia kwa afisa wa Sumatra Mkoani Katavi Bw.Amani Mwakalebela wamesema wao zuio likpo palepale na kukanusha madai uya uongozi wa madereva wa bajaji kuwa wameruhusiwa kufanya safari.
Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri wa majini na nchi Kavu Sumatra,juzi ilikuwa imetangaza kuzuia waendesha bajaji kusafirisha abiria kupitia barabara kuu zinazotumiwa na magari kuanzia jana Agosti 8,2017 hali ambayo ilisababisha kuanzia juzi waendesha bajaji Manispaa ya Mpanda kutangaza mgomo usiokuwa na kikomo mpaka watakaposikilizwa.
Katika mgomo huo uliodumu kwa siku mbili wagonjwa,wajawazito na wazee ni miongoni mwa makundi ambayo yaliathiriwa na mgomo.
Habarika zaidi na www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA