WAKAZI MTAA WA MSASANI MKOANI KATAVI WAONGEZEWA MUDA WA KUONDOKA KUPISHA HIFADHI YA RELI MPANDA-Julai 14,2017

WAKAZI wa mitaa ya Msasani na Tambukareli Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wameongezewa miezi sita badala ya siku 30 walizokuwa wamepewa ili wawe wameondoka ndani ya mipaka ya hifadhi ya Reli.

Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani Bw.Jonad Makoli,muda huo umeongezwa kufuatia kikao cha juzi kilichowakutanisha Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga,viongozi wa mtaa na uongozi wa shirika la Reli Tanzania Mkoani Katavi.
Aidha Bw.Makoli amesema Wilaya ya Mpanda inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutafuta viwanja vyenye bei nafuu kwa ajili ya watakaobomolewa makazi yao pamoja na kuondoa utata wa mita halali za hifadhi ya reli.
Hata hivyo wakazi wa mtaa wa msasani wamesema kuwa hawana uwezo wa kulipia kiwanja kwa shilingi laki tisa walizoambiwa ambapo wameiomba serikali kutazama namna ya upatikanaji wa viwanja kwa shilingi laki moja hadi mbili fedha ambayo ipo ndani ya uwezo wao kulingana na hali ya uchumi wao kwa sasa.
Miongoni mwa athari zitakazojitokeza ikiwa ubomoaji utattekelezwa ni pamoja na upotevu wa mali za familia,familia nyingi kulala nje na watoto kupoteza masomo kutokana na kupelekwa mbali na shule walizokuwa wakisomea.
Wakazi wa Msasani na Tambukareli walikuwa wameamriwa kuondoka ifikapo Julai 28 mwaka huu,ambapo zaidi ya nyumba 200 zinatarajiwa kubomolewa.
Habari zaidi bonyeza p5tanzania.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA