MKUU WA WILAYA YA MPANDA LILIAN MATINGA AMWAGIZA MKURUGENZI MTENDAJI MANISPAA YA MPANDA KUTAFUTA VIWANJA KWA AJILI YA WAKAZI WA MTAA WA MSASANI KABLA YA BOMOA BOMOA-Julai 21,207

MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga,amemwangiza Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,kutafuta viwanja kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msaani kata ya Mpanda Hotel watakaobomolewa makazi yao kabla ya miezi sita waliyopewa kwisha.
Katika picha kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda B.Lilian Charles Matinga(Picha na .Issack Gerald)


Bi.Matinga ametoa agizo hilo leo katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mpanda Hotel katika viwanja vya shule ya Sekondari Kashaulili.
Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya amesema serikali imezuia wakazi kufanya shughuli yoyote katika eneo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania lilipo Manispaa ya Mpanda.
Nao,wakazi wa mtaa wa Msasani wameomba kupewa viwanja kwa bei nafuu kulingana na hali ngumu ya maisha waliyonayo kawa sasa,ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bw.Leonard Kilamhama pamoja na mambo mengine,amesema manispaa ya Mpanda italifanyia kazi haraka suala la wakazi wa mtaa wa msasani kabla ya hatua ya bomoabomoa itakalosababisha zaidi ya nyumba 200 kubomolewa mwezi Januari mwakani.
Shirika la reli Tanzania TRL,wiki iliyopita lilitoa tamko kuwa hakuna mkazi yeyote atakayebaki akiendelea kuishi katika eneo la hifadhi ya reli ambapo hata hivyo utata ambao bado upo ni mita ngapi ambapo kwa sasa zinatajwa mita 30,75 na 215 ambapo mita halali hazijajulikana.

Habarika zaidi P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA