KATA YA MPANDA HOTEL ILIYOPO MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI KUTUMIA SHILINGI MILIONI 21.1 KUMALIZA TATIZO LA MAJI KATIKA MITAA YAKE-Julai 22,2017

KATA ya Mpanda Hotel iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imepata shilingi milioni 21.1 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la maji ambalo limeikumba kata hiyo kwa muda mrefu.

Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara ambao umefanyika kata ya Mpanda Hotel,Diwani wa Kata hiyo Mh.Willium Liwali,amesema kiasi hicho kimetengwa na serikali ili kusaidia kumaliza tatizo la maji katika kata hiyo.

’Kwa kweli Mkuu wa Wilaya hali ni mbaya katika kata ya Mpanda Hotel ambapo tatizo kubwa lililopo kuliko yote katika Mitaa ya Mpanda Hotel,msasani na Tambukareli ni maji ambapo tari tuna milioni 21.1 kwa ajili ya kujenga magati uli kupata maji ya kutosha kuhudumia wakazi zaidi ya 11,000 waliopo kata ya Mpanda Hotel’’.

Aidha Mh.Liwali amesema kata ya Mpanda Hoteli imekuwa na tatizo la utengenezaji wa barabara ambayo imesababishwa na maeneo hayo kuwa bado hayajapimwa ambapo pia amesema ukosefu wa kituo cha huduma za afya kwa wakazi wa kata ya Mpanda Hotel limekuwa tatizo.

Kata ya Mpanda Hotel inaundwa na mitaa mitatu ambayo ni Mpanda Hotel,Msasani na Tambukareli ambayo kwa ujumla ina wakazi zaidi ya elfu kumi na moja.


Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA