DC MPANDA ATAKA VIONGOZI NGAZI ZOTE KUSHIKAMANA PAMOJA KUSUKUMA GURUDUMU LA MAENDELEO-Julai 31,2017



MKUU wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi.Lilian Matinga,amewataka viongozi wote wilayani Mpanda kushikamana kwa pamoja katika kusukuma maendeleo ya Mkoa wa Katavi.

Matinga ametoa wito huo leo katika mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani mkutano ambao umefanyika ukiwashirikisha wataalamu mbalimbali wa Manispaa ya Mpanda.

Katika hatua nyingine,mkuu wa Wilaya ameitaka Halmashauri pamoja na viongozi wa kata kuhakikisha wajasiliamali waliokpoeshwa mikopo wanarejesha kwa wakati ili kunufaisha vikundi vingine ambapo pia ametaka sheria zitumike kuwabana wanaokwepa kurejesha mikopo kwa makusudi.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani Manispaa ya Mpanda wameelezea kusikitishwa na hali inayopelekea wanafunzi wa shule za msingi kuanguka mara kwa mara wanapokuwa wamekunywa dawa ya chanjo kwa ajili ya magonjwa mbalimbali.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu amesema serikali haiwezi kutoa dawa kwa ajili ya kuathiri watoto bali ni maudhi madogomadogo yasiyokuwa na madhara makubwa yanayotokana na dawa hizo.

Mambo mengine ambayo yamejadiliwa katika mkutano mkuu ni suala la upimaji wa viwanja,baadhi ya walimu kutolipwa mishahara kwa wakati na mikopo kwa ajili ya vikundi vya wajasiliamali kwa wanawake na vijana.

Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA