MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 56.75 KWA VIKUNDI VYA WAJASILIAMALI



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi (Februari 5,2017
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Mbwana Mhando,amekabidhi hundi ya shilingi milioni 56,750,000 ambayo ni mkopo kwa vikundi 32 vya wajasiliamali katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando (Mwenye shati nyeupe pichani) akikabidhi mfano wa hundi ya mkpo kwa wajasilimali mbele ya ofisi za kata ya Kabungu.PICHA NA Issack Gerald Februari 5,2017
                                             

Akikabidhi hundi hiyo katika Ofisi za Kata ya Kabungu kwa vikundi vya Mshikamano,Muungano na Ibambye kwa niaba ya vikundi vingine vilivyopo katika Halmashauri hiyo,Mkuu wa Wilaya ameviagiza vikundi vitakavyokabidhiwa mikopo hiyo kuitumia katika malengo yaliyokusudiwa.
Mkuu wa Wilaya kabla ya kukabidhi hundi hiyo,amekagua mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji wa kikundi cha Ibambye na kushiriki kupalilia karanga za kikundi hicho .
Aidha Mkuu wa Wilaya mbali na kukabidhi mbegu ya alizeti kwa kikukndi cha Ibambye pia ameahidi kukipatia kikundi hicho bati 10 kwa ajili ya kuendeleza ufugaji wa kuku.
Kwa uapnde wake Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Raymond Fabian Kashindya amesema,kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri kupitia idara ya maendeleo na ustawi wa Jamii imetoa mkopo wa Shilingi Milioni 56,750,000 kwa vikundi vya wajasiliamali katika mwaka huo wa fedha.
Kashindya amesema jumla ya vikundi ambavyo vimepewa mkopo ni 24 kwa upande wa Wanawake vikiwa na wajasiliamali 119 na vikundi 8 vya vijana vyenye wajasilimali 46 ambapo kwa upande wa wanawake wamepata shilingi milioni 33,350,000 huku vijana wakipata shilingi milioni 23,400,000.
Kwa upande wao baadhi ya wajasiliamali waliopokea mkopo huo wamesema,mkopo unatarajiwa kuwanufaisha na hatimaye kujikwamua kiuchumi.
Hata hivyo watumishi wa umma wakiwemo maafisa ugani na ustawi wa jamii wametakiwa kuwaelimisha wananchi katika sehemu za kazi kuliko kusubiri kufuatwa na wananchi ofisini.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA