YA WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA KAVUU MKOANI KATAVI ISIKUPITE HII HAPA


Na.Issack Gerald Bathromeo-Rukwa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kavuu linalojengwa na kampuni ya Nandra Engineering and Construction Ltd ya mkoani Morogoro na kumtaka mkandarasi huyo kulikamilisha haraka.
Daraja la Mto Kavuu linalojengwa(Na.Issack Gerald)
                                          

Ujenzi wa mradi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 85.34 ulianza Septemba 2013 na ulitarajiwa kukamilika Septemba 27, 2014.Mradi huo wenye thamani ya sh. Bilioni 2.718 unagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo (Jumanne, Agosti 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Majimoto, Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kujiepusha na matapeli wanaopita katika maeneo yao na kuwataka wachange fedha za kuanzisha vikundi ili wapewe sh. milioni 50 zilizoahidiwa na Serikali.
Awali mbunge wa jimbo la Kavuu, Dk. Pudensiana Kikwembe alimuomba Waziri Mkuu kutoa kipaumbele kwenye ujenzi wa daraja la Kavuu ili likamilike mapema na kuwawezesha wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi.
Pia ameiomba Serikali kutekeleza ahadi ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli ya ujenzi wa barabara ya kutoka Majimoto hadi Inyonga yenye urefu wa kilomita 130 kwa kiwango cha lami aliyoitoa wakati wa kampeni. Waziri Mkuu amesema barabara hiyo itajengwa katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Katavi, Mhandisi Abdon Maregesi akizungumzia maendeleo ya mradi wa ujenzi wa daraja la Kavuu amesema umekamilika kwa asilimia 50 na unategemea kukamilika Novemba 30 mwaka huu.
Amesema utekelezaji wa mradi huo umekuwa na kasi ndogo kwa sababu ya uhaba wa fedha, ambapo tangu mwaka ulipoanza hakuna fedha zilizotolewa kwa miaka miwili mfululizo (2013/14 na 2014/15) licha ya kuwekwa kwenye bajeti.
Mhandisi huyo amesema hadi kufikia Agosti 22, 2016 tayari mkandarasi amekwishalipwa jumla ya sh. bilioni 1.284 ikijumuisha na malipo ya awali. Malipo hayo ni sawa na asilimia 47 ya mkataba
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA