WAKAZI WA KATA YA KAYENZE MKOANI MWANZA WAOMBA KUJENGEWA SEKONDARI YA KATA.


Na.Albert Kavano-Mwanza.
Wakazi wa Kata ya Kayenze Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wameiiomba serikali kuwajengea shule ya sekondari ya kata  kutokana na wanafunzi kutembea umbali wa zaidi kilometa 10 kutafuta elimu  kata jirani ya Sangabuye.
Mandari Jiji la Mwanza
                                 

Hayo yamebainishwa juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa wa Iseni katani humo agenda kuu ya mkutano ikiwa kujadili maendeleo ya mtaa huo ikiwemo suala la elimu.
Bi Mariamu Daudi na Bw Josephati Lazaro wamesema  watoto wao wanakumbwa na athari nyingi  kutokana na kukosa shule maeneo ya karibu ikiwemo wanafunzi wakike kubeba ujauzito kutokana  na ulaghai wa wapanda pikipiki ( bodaboda).
Aidha diwani wa kata hiyo Bw James Katoro amesema kuwa lipo eneo la Chasubi  lilotengwa  kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo lakini kamati na uongozi wa serikali iliyopita waliuza eneo hilo kinyemela na amewataka  walionunua eneo hilo kusitisha ujenzi mara moja.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA