UKOSEFU WA MAJI,VITUO VYA AFYA,BARABARA MBOVU NA WATOTO KUTEMBEA KWENDA SHULENI UMBALI MREFU VYAENDELEA KUWATESA WANANCHI VIJIJI VYA TUMAINI NA ITENKA


Vifusi vya udongo vilivyopo barabara inayotoka Kijiji cha Itenka kuelekea Kijiji cha Tumaini inayokarabatiwa(PICHA NA.Issack Gerald
Kisima cha maji kilichopo Shule ya msingi Itenka kinachotegemewa pia na wananchi(PICHA NA.Issack Gerald)
Maji yanayotumika kwa kunywa na shughuli nyinginekijiji cha Tumaini
Wanawake kijiji cha Tumaini wakichota maji maji wakieleza kuwa ni ya kunywa(PICHA NA.Issack Gerald)
Bw.Bulu Bukwaya Mwenyekiti kijiji cha Tumaini(PICHA NA.Issack Gerald)
Bw.Marco Katambi mwenyekiti wa kijiji cha Itenka A(Picha na Issack Gerald)


Na. Issack Gerald Bathromeo
Wakazi wa vijiji vya Tumaini na Itenka A vilivyopo kata ya Itenka Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo,wameiomba serikali kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo ukosefu wa maji safi na salama,ukosefu vituo vya afya pia mindombinu mibovu ya barabara iliyopo.

Wakazi hao wakizungumza katika vijiji hivyo,wamesema ni wakati wa serikali kutekeleza ahadi ilizoziahidi wakati wa kampeni za uchaguzi na kutambua kuwa huduma ya maji na afya ni wajibu wa serikali kuwapelekea wananchi.
Kwa upandewake mwenyekiti wa kijiji cha Tumaini Bw Bulu Bukwaya pamoja na mambo mengine ameiomba Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo kusambaza vifusi vya udongo vilivyolundikwa barabarani bila kusambazwa visambazwe ili kupunguza adha wanazozipata wananchi wanaposafiri kutoka Tumaini kwenda Itenka ambapo vifusi hivyo vinaanzia Itenka kupita kijiji cha Tuamaini.
Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Itenka Bw.Marco Katambi amesema kuwa mpango uliopo kwa sasa ni kujenga madarasa katika shule ya msingi Itenka A pamoja na ujenzi wa kituo cha Polisi kijijini hapo ambapo kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji hicho askari hawapo kijijini hapo kufanya ulinzi mara kwa mara.
Hivi Karibuni diwani wa kata ta Itenka Bw.Joseph Raulence Mpemba alikiri kuwepo kwa chanagamoto mbalimbali kwa kata nzima ya Itenka yenye vitongoji 26 ambapo alisema changamoto kubwa zilizopo ni uhaba wa madarasa kwa shule ya Msingi Itenka,watoto kutembea umbali mrefu kwenda shule,matatizo ya maji,miundombinu mibovvu ya barabara,Ukosefu wa kituo cha afya na matatizo ya maji.
Hata hivyo Bw.Mpemba alisema kuwa katika sekta ya afya zimetengwa Shilingi milioni 70 kujenga kituo cha Afya kijijini Itenka kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Vijiji hivyo umaarufu wake ni kilimo cha Mpunga na ufugaji wa ng’ombe
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA