MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AZIAGIZA MAMLAKA ZA ARDHI VIJIJI VYA KAMILALA NA KATUMA KUWEKEANA MIPAKA YA KUDUMU KUONDOA MIGOGORO YA ARDHI.



Na.Judica Sichone-Tanganyika
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Saleh Mhando aziagiza mamlaka za ardhi katika kijiji cha Kamilala na Katuma kuhakikisha wanaweka mipaka ya kudumu haraka iwezekanavyo ili kuondokana na migogogro ya ardhi.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi katika vijiji hivyo juu ya mgogoro wa ardhi unaoendelea katika vijii hivyo ikiwa chanzo ni ukosefu wa mipaka.
Ameahidi kushughulikia kwa haraka mgogoro huo kabla ya msimu wa kilimo haujaanza ili mwenye haki aweze kuendelea na shughuli za kilimo na kuwasihi wasijichukulie sheria mkononi pasipo kufuata sheria.
Nao baadhi ya wananchi katika vijiji hivyo wamefurahia ujio huo wa mkuu huyo wa wilaya ya Tanganyika na kuwa hiyo ni moja ya njia ya usuluhishi wa mgogoro huo.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA