BREAKING NEWS:SERIKALI YA WILAYA YA TANGANYIKA YAOMBA RADHI MAMA MJAMZITO KUJIFUNGULIA NJE AKIWA MBELE ZAHANATI IKIWA IMEFUNGWA


Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika
Serakali ya wilaya ya Tanganyika imeomba radhi wakazi wa kijiji na kata ya Ipwaga kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kwa kitendo cha mama mjamzito kujifungulia nje akiwa mbele ya zahanati baada ya kufikishwa kituoni hapo kutokana na kituo hicho kufungwa na muuguzi akiwa hayupo.
                                          
Zahanati ya Ipwaga ambayo mama mjamzito alijifungulia nje baada ya kufikishwa hapo(PICHA.Issack Gerald)

Tamko la wananchi hao kuombwa radhi na serikali limetolewa na mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando kwa niaba ya serikali ya Wilaya ya Tnganyika wakati akizungumza na wakazi wa kijiji na kata ya Ipwaga.
Amesema kuwa serikali imekiri kukosea akisema kuwa muunguzi aliyekuwepo alikuwa amepeleka mafaili Hospitali ya Wilaya Mpanda na zahanati kukosa mtu aliyetakiwa kuwepo na kupelekea tukio hilo kutokea.
Taukio la mama kujifungulia nje ya Zahanati lilitokea Agosti 1 mwaka huu likimhusisha mwanamke mjamzito aliyetambulika kwa jina la Neema Sostene(31) kutoka kijiji cha Mwibasi.
Hata hivyo hatua ya Bw.Ngalinda Ahmada  ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Kumpatia barua ya Onyo Muuguzi huyo kilionekana kuwakwaza baadhi ya wananchi waliokuwepo katika mktano wakidai kuwa ni vema serikali ndiyo ingewajibika na siyo kumwajibisha muuguzi huku wakitambua kuwa yupo peke yake ambapo anatakiwa kufanya kazi mbalimbali zikiwemo kupima wagonjwa,kutoa dawa kwa wagonjwa,kusaidia wanawake wajawazito wanaotaka kujifungua na kufanya kazi za kiofisi.
Wakati huo huo  zahanti hiyo imeongezewa muuguzi mwingine ili kusaidia huduma mbalimbali katika zahanati hiyo ikiwemo kusaidia akina mama wajawazito wenye uhitaji wa kujifungua ambapo muuguzi huyo ametolewa katika kituo cha afya Mishamo.
Wengine ambao Mkurugenzi alisema lazima wawajibishwe ni Maafisa watendaji wa kijiji  na kata na Diwani kwa kutotoa taarifa katika mamlaka husika mpaka Mkurugenzi mwenyewe alipopata taarifa kutoka kwa raia.
Kwa upande wake Muuguzi huyo aliyepewa onyo,amekiri kutokuwepo katika zahanati akidai kuwa alikuwa amepeleka nyaraka Mpanda Mjini alizokuwa ameagizwa na Viongozi wake aziwasilishe ambapo hata hivyo amekanusha taarifa zilizotangazwa na Shirika la Utangazaji TBC kuwa hakuwepo katika kituo cha kazi kwa siku nyingi.
Hata hivyo zahanati hiyo bado in changamoto ya upungufu wa vitanda vya kujifungulia wajawazito.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habrika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA