MWENGE WA UHURU KUANZA MBIO ZAKE WILAYANI KIBONDO



Leo Mwenge wa uhuru unaanza mbio zake Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2016 Bw.George Mbijima(PICHA NA Issack Gerald)
                                

Mwenge wa uhuru ukiwa Wilayani humo unataraji kuzindua miradi mbalimbali yenye Thamani ya zaidi ya shilingi Millioni 900.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kibondo Bw Saidi Shemahonge amesema mpaka kufikia jana maandarizi ya kupokea mwenge huo pamoja na miradi itakayo zinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi na mbio za mwenge yalikuwa yamekamilika.
Bw Shemahonge amesema miradi itakayowekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa  na mbio hizo za mwenge ni pamoja miradi iliyo chini ya serikari pamoja na watu binafisi  sambamba na miradi ya vikundi maalumu hususani vijana na wanawake
Aidha Bw Shemahonge ametoa wito kwa watu wote  ambapo mwenge huo utapita kujitokeza kwa wingi kuulaki na kusikiliza ujumbe mbalimbali unaotolewa kwa lengo la kuhimiza maendeleo.
Halmshauri ya Wilaya ya Kibondo ni miongoni Wilaya 6 zinazounda mkoa wa Kigoma ambapo wilaya nyingine ni BUHIGWE, KAKONKO, KASULU,  KIBONDO KIGOMA  na UVINZA
Mwandishi: Jastini Cosmas-Kibondo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA