BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO LAFANYA KIKAO CHA MWISHO KUHITIMISHA MWAKA WA FEDHA 2015/2016,MWENYEKITI WA HALMASHAURI ATOA NENO KWA MADIWANI.



Na.Judica Schone-Nsimbo
Madiwani wa baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo na viongozi wa halmsahauri hiyo waliopewa dhamana ya kukusanya mapato katika halmashauri hiyo,wametakiwa kusimamia zoezi la ukuasanyaji wa mapato ili kutumika kwa mujibu wa bajeti.

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya hiyo  Mh Raphael Kalinga katika kikao cha mwisho cha madiwani kwa mwaka wa fedha 2015/2016  Kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Bw Kalinga amesema mwaka wa fedha 2016/2017 halmashauri imepewa dhima ya ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao,hivyo ni vema kuwa waaminifu katika zoezi hilo kwani atakayebainika kuhusika na matumizi binafsi ya mapato hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Katika hatua nyingine Kalinga amewataka baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiwashawishi wananchi kutochangia maendeleo katika maeneo yao kuacha mara moja kwani maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe.
Aidha ameonya tabia ya baadhi ya watumishi katika halimashauri hiyo wanaotoa huduma kwa ubaguzi na kupigiwa magoti na wateja wao kuacha mara moja kwani ni haki yao kupatiwa huduma pasipo usumbufu wowote.
Nao baadhi ya madiwani katika halmashauri hiyo  wamesema kuwa changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili katika kata  na halmashauri zao ni pamoja na akina mama wajawazito kujifungulia majumbani na chanzo kikiwa ni akina mama kuwategemea zaidi wakunga waliopo majumbani ambao hawana uwezo mkubwa kwa kitaaluma.
Katika hatua nyingine,wamesema kuwa wanatarajia kuanzisha chama cha msingi cha ushirika kwa wakulima wa zao la tumbaku katika Halmshauri ya Wilaya ya ili kuwasiadia wakulima na kuongeza mapato ya Halmashauri,
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA