BARABARA YA MPANDA TABORA KUPITIA MTO KOGA YAFUNGULIWA



BARABARA inayoanzia Mpanda hadi Tabora kupitia daraja la mto Koga imefunguliwa na magari kuruhusiwa kutumia barabara hiyo kwa safari.

Kufunguliwa kwa barabara hiyo iliyokuwa imefungwa tangu Januari 28 mwaka huu,kumetangazwa na Naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia miundombinu nchini Mh: Suleiman Moshi Kakoso.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini amesema barabara hiyo imefunguliwa baada ya Kukamilika kwa Ujenzi wa Daraja la Mto Koga lililokuwa limesombwa na Maji Kufuatia Mvua zilizokuwa zikiendelea Kunyesha na kusababisha vifo vya watu 10.
Kufunguliwa kwa barabara hiyo kutaondoa adha kwa wasafiri na wamiliki wa vyombo vya Usafiri waliokuwa wakilazimika Kupitia Mkoani Kigoma kwenda Mkoani Tabora hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa na Wananchi.
Awali taarifa za kufunguliwa kwa barabara hiyo zilikuwa zimetolewa Jana na Nasoro Alfi  ambaye ni Kamati ya Usalama barabarani Mkoani Katavi ambapo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi kuwa ujenzi wa daraja la mto Koga umekamilika na magari yanaruhusiwa.
,Mwenyekiti wa Kamati hiyo Nasoro Alfi aliesema barabara hiyo imefunguliwa baada ya Kukamilika kwa Ujenzi wa Daraja la Mto Koga lililokuwa limesombwa na Maji Kufuatia Mvua zilizokuwa zikiendelea Kunyesha.
Daraja la Mto Koga ni Kiunganishi cha Mikoa ya Katavi na Tabora ambapo Kufunguliwa kwake kutayafanya Mabasi ya abiria kuanza kupitia barabara tofauti na ilivyokuwa awali ambapo yalilazimika Kupitia Uvinza Mkoani Kigoma.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo  
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA