MBUNGE JIMBO LA MPANDA VIJIJINI ALINDIMA BUNGENI DODOMA KUTETEA VITUO VYA AFYA JIMBONI KWAKE



VITUO vya afya vya Mwese,Karema na Mishamo Wilayani Mpanda Vinakabiliwa na ukosefu wa wataalaamu wa afya na gari la wagonjwa-leo Mbunge Jimbo la Mpanda Vijijini Mh.Suleiman Kakoso alindima bungeni kutetea vituo hivyo.

Hali hiyo imeibuka wazi leo kufuatia Swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Bw Suleiman Kakoso lililo hoji je  ni lini serikali itavipatia  mahitaji hayo vituo hivyo ili kuokoa maisha ya wananchi.
Akijibu swali hilo waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Bw George Simba Chawene amesema serikali kwa sasa haina mpango mahususi wa kununua magari ya wagonjwa  kwa nchi nzima isipokuwa wanangalia bajeti ya halimashauli zao.
Aidha Chawene amesema sehemu ya kuanzia kukamilisha huduma mbambali katika sekta za elimu pamoja na afya mipango hiyo huanzia katika halmashauli.
Mbali na chanamoto hizo katika vituo hivyo,pia vituo hivyo na vinginevyo katika jimbo hilo vimekuwa vina matatizo ya ukosefu wa huduma ya maji ya uhakika kikiwemo kituo cha afya cha Mwese.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA