JIONEE HII KALI: WAKAZI MTAA WA MSASANI MANISPAA YA MPANDA WATESWA NA KUNGUNI,WAOMBA SERIKALI IWASAIDIE DAWA YA KUWAUA


Katika hali isiyokuwa ya kawaida,wakazi wa Mtaa wa Msasani Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwasaidia kupatikana dawa ya kuua wadudu aina ya KUNGUNI ambapo walisema kuwa wameshindwa kupata hata usingizi usiku.
                                             




Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda Radio Fm,walisema kuwa wametumia dawa ya kila aina lakini wadudu hao wameshindikana kuuwawa na kutokomezwa kabisa.
Baadhi ya wakazi waliozungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti kuhusiana na hali hio ni pamoja na Zabibu Said(56),Philbert John(36),Elisha Kenya(47),Taus Jimack(28) ambao walisema kuwa tatizo la kunguni limeathiri hata wanafunzi kwani wanasinzia darasani wanapokuwa wanasoma ambapo usingizi unasababishwa na kutolala usiku kwa sababu ya wadudu hao.
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa serikali ya mtaa huo Bi.Fortunata Willium alithibitisha kuwepo kwa kunguni hao katika mtaa huo hata nyumbani kwake ambapo alisema kuwa wamezungumza ili serikali iwapatie msaada wa dawa ya kuua wadudu hao wakorofi.
Hussein Jamli Kweka mmoja wa wamiliki wa nyumba za kulala wageni maarugu kama GUEST katika Manispaa ya Mpanda,yeye ni mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ya Grali Lodge(TWO IN ONE) alithibitisha kuwepo kwa kunguni katika mtaa wa Msassani na hata katika nyumba zake za kulala wageni ambapo alisema kuwepo kwa kunguni katika nyumba yake ya kulala wageni kumemuathiri katika suala la kipato ambapo wateja wengi wamekuwa wakikimbia kutokana na wadudu hao kuwa wasumbufu kwa wageni wanaolala mahali hapo.
Hata hivyo chanzo cha wadudu hao kinasemekana ni kuwepo kwa uchafu ndani ya nyumba hususani katika vitanda vya kulalalia licha ya kuwa halijathibitishwa na wataalamu wa afya.
Idadi kubwa ya wakazi waliozungumza na Mtandao huu sanjari na  Mpanda Radio walitaja vyandarua vya msaada kuwa chanzo cha kunguni hao kwa kuwa vyumba ndani ya nyumba au wakazi wasiotumia vyandarua hivyo hawana kunguni ndani ya nyumba hata mmoja ambapo waliongeza kuwa kabla ya kugawiwa vyandaru ahivyo kunguni hawakuwepo.
Miongoni mwa dalili na madhara ya kunguni ni pamoja na Ugonjwa wa mabaka mwili mzima,Upungufu wa hewa,Kufura macho,Kusokotwa na tumbo
Mawasiliano kati ya Idara ya Afya na waandishi wa habari yanaendelea ili kuliangazia suala hili ikiwa kuna uwezekanao wa kuwasaidia wakazi hao.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM usikose mwendelezo wa suala hili kupitia hapahapa

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA