IDADI YA WATUMISHI HEWA YAZIDI KUPANDA KATAVI KUTOA 21 MWEZI ULIPOITA SASA 46 SERIKALI YAPATA HASARA ZAIDI YA MILIONI 200,MKUU WA MKOA WA KATAVI ATOA SIKU SABA KWA MKURUGENZI KUWAFUKUZA KAZI WATUMISHI HEWA



IDADI ya Watumishi hewa Mkoani Katavi imeongezeka Kutoka 21 ya awali na kufikia watumishi hewa 46 walioisababishia Serikali hasara ya Shilingi Milioni 200,792,448.


Akizungumza na wandishi wa  habari ofisini kwake  Mapema  leo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ametoa siku 21 kwa Wakurugenzi wa halmashauri Kuwajibika Kuzirudisha fedha za Umma zilizotumika kuwalipa watumishi hao hewa.
Meja Jenerali Muhuga amesema Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ambayo awali haikuwa na watumishi hewa imeongoza kwa kuwa na idadi ya watumishi hewa 16 walioisababishia Serikali hasara ya shilingi Milioni 31,231,516.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambayo awali ilikuwa na watumishi hewa 17 Imeshika nafasi ya pili kwa kuwa na Watumishi hewa 11 Walioisababishia Serikali hasara ya Shilingi Milioni 90,641,880.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Katika Mkoa wa Katavi, watumishi waliokufa wanaoendelea kulipwa mishahara ni 5,Waliostaafu ni 19,walioacha kazi kwa hiari 1,waliokuwa na mishara miwili -2,Watoro Sugu ambao hawapo vituoni 13, vyeti vya kughushi ambao baada ya timu kuanza uchunguzi walitokomea kusikojulikana 3 na waliofukuzwa ni 3.
Katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi mpaka sasa,Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeonekana kuongoza kwa kuwa na watumishi hewa 17 kutoka 9 Machi 30 mwaka huu na kuisababishia serikali kupata hasara ya Shilingi Mil.31,231,516/=,ikifuatiwa na Manispaa ya Mpanda yenye watumishi hewa 16 walioisababishia serikali hasara ya shilingi Mil.90,641,880 ambapo katika Ripoti ya Aprili 21 mwaka huu ilisema kuwa haikuwa na mtumishi hewa hata mmoja,Mlele ina watumishi hewa 10 kuotoka 2 machi 31 ambapo hiyo ni sawa na hasara ya Shilingi Mil.45,650,900/=huku Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda ikiwa na watumishi hewa 09 walioisababishia hasara ya shilingi Mil.33,268,152 na kufanya JUMLA KUU ya hasara ya fedha za serikali katika Mkoa wa Katavi kuwa MIL.200,792,448
Hata hivyo pamoja na kuishukuru timu kwa uchunguzi mzurzi,Mkuu wa Mkoa ametoa siku 21 kwa wakurugenzi wa halmashauri zote Mkoani Katavi kuhakikisha fedha zote zinarudishwa huku akitoa siku 7 kwa wakurugenzi hao kufuta watumishi hewa wote.

Mwandishi :Meshack Ngumba
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA