DIWANI NA MWENYEKITI WA KIJIJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WATAKIWA KUACHA TOFAUTI ZAO ZA KISIASA,WAANDISHI WA HABARI KUFUKUZWA MKUTANO WA HADHARA WANANCHI WANG'AKA



Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imewataka Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Bw Makalai Njile na Diwani wa Kata ya ibindi Mh, Justin  Shinje Kuachana na Chuki za Kisiasa na badala yake wafanye kazi ya kutatua kero za wananchi wao.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh Raphael Kalinga wakati akitolea ufafanuzi Kuhusu  Mgogoro uliopo wa wananchi Kumkataa  Mwenyekiti wa Kijiji hich.
Katika hatua nyingine Mh,Kalinga amesema kitendo cha kuwazuia wandishi wa habari Kufika Katika Mkutano wa hadhara wa Kijiji hicho uliofanyika May 21 Mwaka huu na diwani wa Kata hiyo Kinapingana na haki ya kikatiba kupokea na Kutoa habari kwa umma kupitia vyombo vya habari hapa nchini.
Aidha Mh,Kalinga amesema  tayari Mgogoro uliopo baina ya Mwenyekiti wa Kijiji hicho na Diwani wa Kata ya Ibindi Ulishafikishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mlele tayari kwa Kufanyiwa Kazi.
Hata hivyo Mh,Kalinga amesema bado mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Bw,Makalai Njile anatambulika Kisheria kama mwenyekiti halali.
Kwa upande wa wananchi waliokuwepo katika mkutano,wameelezwa kutoridhishwa na kitendo cha diwani wa kata hiyo kuwazuia waandishi wa habari kushiriki kuandika habari za mkutano huo licha ya kuwa mwenyekiti wa kijiji ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka ya kuitisha mkutano kuwa na taarifa za uwepo wa mwaandishi wa habari.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA