ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 3 KUTUMIKA KUJENGA HOSPITALI YA MKOA WA KATAVI



SERIKALI ya mkoani katavi imeazimia  kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya   kuanzisha ujenzi wa hospitali ya mkoa.

Hayo yamebainishwa jana na mkuu wa mkoa wa katavi meja jeneral Raphael Muhuga wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika  katika viwanja vya maridadi manispaa ya Mpanda.
Muhuga amesema kuwa  haospitali ya wilaya ya Mpanda haitoshi  ukilinganisha na mahitaji ya watu  ambapo katika vikao vya bajeti imepewa kipaumbele.
Aidha amesema vituo vya afya vitaboreshwa ambavyo viko nje ya manispaa ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya.
Kwa sasa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda inatoa huduma kwa wakazi wote Mkoani Katavi ikibeba jukumu kama Hospitali ya Mkoa ambapo changamoto kubwa ambazo zimekuwa zikiibuka katika hospitali hiyo ni msongamano wa wagonjwa usioendana na miundombinu na upungufu wa dawa na vifaa tiba.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA