RAIA WAPYA KATUMBA NA MISHAMO WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA VITENDO VYA UHARIFU.



Raia wapya waishio makazi mapya ya Katumba na Mishamo wametakiwa kutojihusisha na vitendo vya uharifu na badala yake wametakiwa kufuata sheria za nchi.

Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa shirika la kuhudumia wakimbizi duniani hapa nchi Tanzania Bi.Chansa Kapaya wakati wa makabidhiano ya vyumba vine vya madarasa,nyumba moja ya mwalimu katika shule ya sekondari Mazwe na bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari Mishamo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mazwe Mwl. Oswadi Sabasi Masawe anaona kwa upande wake nyumba na madarasa ni mkombozi kwa walimu na wanafunzi.
Shule ya Sekondari Mazwe ina wanafunzi 189 wa kidato cha kwanza kati ya 250 wanaotakiwa kuwepo shuleni hapo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA