MTOTO MWENYE ULEMAVU WA VIUNGO ATUNZWA NDANI YA NYUMBA MIAKA MIWILI BILA HATA YA KUPATA MAHITAJI YA MSINGI

Na.Issack Gerald-Katavi
Taarifa iliyopatikana Aprili mosi mwaka huu ni yan mtoto mmoja  mwenye ulemavu wa viungo  katika manispaa ya Mpanda mkoani katavi ambaye amekuwa akifungiwa ndani kwa muda wa miaka miwili na kukosa haki zake za msingi kama elimu wakati mwingine hata chakula.

Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo mama mlezi wa mtoto  Bi Ester Kapandila amesema baba mzazi ndiyo chanzo cha tatizo hilo.
Kutokana na tatizo la mtoto huyo,dada yake aitwaye Christina Mziyuka ambaye ni yeye ni mwanafunzi kwa ajili ya kumhudumia motto huyo.
Mtoto Christina ambaye awali alikuwa akisoma darasa la sita katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Sumbawanga Rukwa,amesema kuwa mama huyo mlezi aliyekuwa akimhudumia mtoto huyo mlemavu baadaye alikatazwa na baba wa mtoto huyo mwenye ulemavu na jukumu la matunzo kupewa dada yake mwanafunzi na kupelekea mwanafunzi kusitsha masomo ili kumhudumia kaka yake.
Kwa upande wake  afisa ustawi wa jamii Bi ledy Gunda  amesema mtoto huyo amekuwa akitengwa na kunyimwa fursa kama watoto wengine.
Aidha ametoa wito kwa  jamii  kutambua haki ya mtoto na kushilikisha vyombo vya kijaamii kwa ajili ya msaada zaidi.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA