WAGONJWA WAANZA KUTEMBEZA KICHAPO KWA WAUGUZI HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA



Na,Meshack Ngumba-Mpanda
KUFUATIA tukio la jana la Muuguzi  Katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda Kupigwa na Mgonjwa aliyekuwa akimuhudumia, Serikali imeshauriwa Kuimarisha Usalama wa watumishi Katika maeneo yao ya Kazi.

Katika hali isiyo ya kawaida imezoeleka kusikia wahuduma wa afya Katika vituo mbalimbali hapa nchini wakilalamikiwa na wagonjwa Kwa Kutumia lugha zisizokuwa na staha,lakini safari hii hali imekuwa tofauti  Kufuatia tukio la Mgonjwa Kumpiga ngumi Muuguzi wa zamu aliyekuwa akimuhudumia Kwa Madai ya Muuguzi Kumtaka Mgojnwa huyo alale Kitanda Kimoja na Mgonjwa Mwenzake.
Bi Recho Matinya ni Muuguzi Katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambaye pia ndiye Mwathirika wa tukio hilo amesema kuwa alipigwa ngumi,ambapo baada ya hali hii ilimlazimu Muuguzi huyu kuiomba serikali Kukomesha Kadhia Kama hii Kutotokea kwa watumishi wengine  wa umma na pia Katika sekta nyingine
Maria Komba ni shuhuda wa tukio hilo kwa upande wake alilaani Kitendo hicho na kuitaka Serikali  iangalia namna ya Kulinda haki za wauguzi akisema kuwa mgonjwa huyo aliamka katika kitanda na kumvagaa muuguzi.
Ni Kipindi cha Wiki Moja Kimepita tangu wabunge wa Viti Maalumu  Mh,Anna Lupembe na Mh Taska Mbogo Kutembelea Hospitali hiyo ili Kujionea Mapungufu yaliyopo lakini hata kabla hawajaingia ndani Kulitokea Mvutano Kuhusu uhalali wa Kufungwa kwa geti la Kuingia Katika hospitali hiyo Muda wote.
Kutokana na tukio hilo la  Mgonjwa Kumpigwa  Muuguzi wakati akimuhudumia anazungumzia ulazima wa Kufungwa kwa geti hilo.
Hivi karibuni waaguzi Mkoani Mwanza walilazimika kugoma kufanya kazi wakishinikiza serikali kuingilia kati wakidai kufanyiwa udhalilishaji ikiwemo kudia kuelekezwa majukumu na wagonjwa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA