VIONGOZI STENDI KUU YA MABASI MANISPAA YA MPANDA WAMWANGUKIA MKUU MPYA WA MKOA KATAVI KUTATUA CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU INAYOWAKABILI,BARABARA KUTOKA MPANDA HADI TABORA BADO PASUA KICHWA


Na.Issack Gerald-Katavi
                                                              


Uongozi wa Stendi kuu ya mabasi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,umemwomba Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Raphael Muhuga kuingilia kati kutatua changamoto ya kutowaka kwa taa za umeme katika stendi tangu mwaka jana pamoja na wasafiri kukosa mahali pa kujikinga mvua na jua.

Ombi hilo limetolewa leo na Mwenyekiti Msaidizi wa Stend Bw. Ramadhani Nkwizu wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sanjari na Mpanda Radio Katika stendi hiyo.
Amesema licha ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda na Mkuu wa Wilaya Mpanda kuahidi kutatua changamoto hiyo tangu mwaka jana,hakuna kilichotekelezeka mpaka sasa.
Kwa upande wake Jailos Kipenye amesema kuwa watu wamehofia kuingiliwa na waharifu pamoja na kuibiwa mali zao kutokana na kutokuwepo kwa mwanga nyakati za usiku.
Suala la barabara kutoka Mpanda Kupitia Tabora ikiwa ni takribani miezi 3 sasa tangu katazo la kutumia barabara hiyo kutumika kutolewa wasafirishaji na wasafiri wanakumbwa na adha ya kutofika Tabora kwa muda mwafaka pamoja  na wasafiri kutumia kiasi kikubwa cha nauli.
Aidha viongozi hao wakamwomba mkuu wa Mkoa kushughulikia tatizo la barabara inayoanzia Mpanda hadi Tabora.
Kufuatia hali ya sintofahamu juu ya hatima ya barabara kutoka Mpanda Kuelekea Inyonga hadi Tabora,Machi 25 mwaka huu,Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara kutoka Mpanda Kuelekea Tabora aliitaka serikali ya Wilaya ya Mlele kuendelea kuzuia magari makubwa yakiwemo ya abiria kutoruhusiwa kupita katika barabara hiyo kwa kuwa msimu wa mvua za masika unaendelea isipokuwa akasema kuwa magari madogo yasiyo ya abiria yanaruhusiwa kupita.
Mto Koga hupokea maji kutoka mito ya Rungwa na Chunya kupitia ziwa Rukwa
Barabara ya kutoka Mpanda Katavi hadi Tabora ilizuiliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Msengi aliyezuia barabara hiyo kutumiwa na vyombo vya usafiri Januari 26 mwaka 2016,kutokana na daraja la mto Koga linalotenganisha Mkoa wa Katavi na Tabora kukatika ambapo jumla ya watu 10 walikufa maji baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA