SERIKALI YA MKOA WA KATAVI YAKATAA WAKANDARASI WASIOFUATA MASHARTI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI.


Na.Issack Gerald-Katavi
SERIKALI Mkoni Katavi imesema haitakubali Kuingia Mikataba ya Ujenzi wa Miradi mbalimbali ikiwemo  barabara  na wakandarasi  wanaoshindwa Kufuata Masharti  ya Utekelezaji wa Miradi hiyo.
                                                
 Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahim Msengi  wakati akizungumza  na wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa mkoani Katavi Katika Kikao cha bodi hiyo kinacholenga Kujadili changamoto za Miundombinu na jinsi ya Kuzitatua.
Katiki Kikao hicho Wajumbe wametoa pendekezo la Kuundwa kwa Kamati itakayofuatilia Ujenzi wa daraja la Mto koga linalounganisha Mikoa ya Katavi na Tabora Kufuatia kuharibiwa na Mvua zinazoendelea Kunyesha na Kusababisha Kukosekana kwa Mawasiliano ya Miundo Mbinu baina ya Mikoa hiyo.
Katika daraja la mto Koga,watu 10 walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria wakati wakitoka Mkoani Tabora kuingia Mkoani Katavi.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kavuu Bi.Pudensiana Kikwembe,ameshauri kuepuka gharama za ulipaji wa fidia zisizokuwa za msingi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA