RAIS MAGUFULI ATEUA WAKUU WAPYA WA MIKOA, WAMO 13 WAPYA,Dk.MSENGI WA KATAVI AONDOLEWA ALETWA RAPHAEL MUHUGA,PAUL MAKONDA AULA DAR


Na.Issack Gerald
Rais wa Tanzania amewateua wakuu 13 wapya wa mikoa miongoni mwa orodha mpya ya wakuu 26 wa mikoa iliyotangazwa leo na ikulu ya rais.
                                                   
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

Rais John Pombe Magufuli amewahifadhi wakuu 13 waliokuwa katika serikali ya Jakaya Kikwete.
Uteuzi huo umetangazwa na katibu mkuu kiongozi, Mussa Ibrahim Iyombe.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliyotiwa sahihi na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika ikulu, Gerson Msigwa, Viongozi hao wote walioteuliwa wataapishwa katika hafla maalum itakayoandaliwa jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa tatu asubuhi jijini Dar es salaam.
Orodha ya wakuu wa mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
ORODHA YA WAKUU WA MIKOA NA MIKOA WANAYOONGOZA
Paul Makonda
Dar es Salaam
Ezekiel Elias Kyunga
Geita
Salum Mustafa Kijuu
Kagera
Raphael Muhuga
Katavi
Emmanuel Maganga
Kigoma
Godfrey Zambi
Lindi
Dkt. Steven Kebwe
Morogoro
Zerote Steven
Rukwa
Anna Malecela Kilango
Shinyanga
Methew Mtigumwe
Singida
Antony Mataka
Simiyu
Aggrey Mwanri
Tabora
Martine Shigela
Tanga
Jordan Mungire Rugimbana
Dodoma
Said Meck Sadick
Kilimanjaro
Magesa Mulongo
Mara
Amos Gabriel Makalla
Mbeya
John Vianey Mongella
Mwanza
Daudi Felix Ntibenda
Arusha
Amina Juma Masenza
Iringa
Joel Nkaya Bendera
Manyara
Halima Omary Dendegu
Mtwara
Dkt. Rehema Nchimbi
Njombe
Evarist Ndikilo
Pwani
Said Thabit Mwambungu
Ruvuma
Chiku Galawa
Songwe (Mkoa mpya)

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA