KUHUSU MADARASA YA WANAFUNZI WENYE WALEMAVU SHULE YA ,MSNGI AZIMIO,SASA SARAKASI TUPU KATI YA MANISPAA YA MPANDA NA MKANDARASI


Na.Issack Gerald-Mpanda
Kamati ya shule ya msingi Azimio katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imezuia malipo ya shilingi Milioni tano (5,000,000) kwa mkandarasi anayefahamika kwa jina la Paul Luguyashi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandoya Investment aliyejenga madarasa mawili ya watoto wenye ulemavu katika shule hiyo kwa madai kuwa sehemu ya majengo hao aliyoambiwa kufanya marekebisho ya majengo hayo hakutekeleza.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio Fm,Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Patrick Julius Mbasha amesema,licha ya Mhandisi  wa Manispaa ya Mpanda kuidhinisha malipo kufanyika na pesa hiyo kuingizwa katika akaunti benki shule ya msingi Azimio,kamati haitaidhinisha pesa hiyo kukabidhiwa kwa mkandarasi huyo hadi hapo atakapofanya marekebisho.
Bw.Mbasha amesema,kucheleweshwa kwa malipo ya fedha hiyo kumetokana na mkandarasi kutofanya marekebisho kama alivyoelekezwa na watalaamu wa ujenzi kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Mwandoya Investment amesema,marekebisho aliyotakiwa kuyafanya alikwishamaliza na kilichokuwa kimesalia ni malipo pekee na ndiyo maana alipewa nakala ya barua ya Februari 8 mwaka huu na kamati kuagizwa kumlipa shilingingi milioni Tano iliyoingizwa katika akaunti benki ya shule.
Hata hivyo kutokana na hali hiyo,mkandarasi hiyo amesema, kutokana na ucheleweshaji wa kumlipa psea yake mpaka sasa pamoja na riba ya malimbikizo ya pesa yote imefikia karibu milioni 33 suala ambalo kamati ya shule imesema haitambui kiasi hicho cha fedha.
Aidha Mkandarasi huyo ameenedelea kusisitiza kufunga madarasa hayo mpaka atakapoliwa pesa yake na akafafanunua kuwa ikiwa suala hili halitakwisha,atalipeleka Wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI kwa hatua zaidi.
Naye Kaimu mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Bw.Hamisi Mkele,amesema suala hilo limebaki mikononi mwa kamati ya shule kulipwa pesa iliyoidhinishwa na Manispaa na akaongeza kuwa ikiwa mkandarasi anadai milioni 33 ikiujumuisha pamoja na riba basi afike Ofisini ambapo kwa mjibu wa maelezo ya mkandarasi,siyo mara ya kwanza kuzungumza nao suala la nyongeza ya riba.
Madarasa hayo mawili ya watoto wenye ulemavu wengi wao wakiwa wa kutosikia yalikamilika kujengwa mwaka 2014 huku maelewano yakiwa ni Shilingi milioni 33 na awali zikawa zimelipwa milioni 26 na kusalia milioni 7 hadi alipofunga madarsa hayo mwaka 2014 akishinikiza kulipwa pesa anayodai.
Wanafunzi hao kuanzia darasa la kwanza hadi la saba kwa miaka 7 tangu mwaka 2007,wanafundishiwa katika darasa moja,ubao mmoja na wakati mwingine walimu zaidi ya watatu kufundisha  kwa wakati mmoja.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA