KAMANDA KIDAVASHARI ATOA KAULI KUHUSU WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA UHARIFU MSIMU WA SIKUKUU YA PASAKA


Na.Issack Gerald-Katavi
JESHI la Polisi Mkoani Katavi limetoa onyo kwa kikundi au mtu yeyote atakayesababisha vitendo vya furugu, fujo ama vitisho vinavyosababisha uvunjifu wa amani katika kipindi chote cha kusheherekea sikukuuu ya pasaka.

Kauli hiyo imetolewa leo na kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ASP Dhahiri Kidavashari wakati akizungungumza na vyombo vua habari kuhusu namna ambavyo jeshi la polisi limejipanga kuimarisha usalama kipindi cha sikukuu pasaka.
Aidha, Kamanda Kidavashari amewasisitiza wazazi/walezi kutowaachia watoto wao wadogo kuzurura ovyo maeneo hatarishi kama vile barabarani,kuogelea kwenye madimbwi ya maji/fukwe au kwenda maeneo ya mbali kutoka wanapoishi ili kuepusha kupotea au kukumbwa na majanga yanayoweza kuepukika.
Wakati huo huo,Kamanda Kidavashari anawaasa madereva wa vyombo vya moto kutokutumia vileo kupita kiasi cha kushindwa

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA