HABARI KUU 6 ZA WIKI ZILIZOTOKEZA KATAVI MACHI 21-27,2016 ,P5 TANZANIA MEDIA INAKUSOGEZEA


WAKAZI WAISHIO MLIMA WA LIAMBA LYAMFIPA WATAKIWA KUHAMA KABLA NGUVU YA JESHI KUTUMIKA.
Na.Issack Gerald-Mlele                                                               
Baadhi ya wakazi waliojenga nyumba na kuanza kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo katika mlima wa Liamba Lyamfipa uliopo Wilayani Mlele Mkoani Katavi wametakiwa kuhama mara moja sehemu hiyo.

Kupitia kilele cha maadhimisho ya siku ya wiki ya maji yalifofikia kilele chake Machi 22 ambayo yalifanyika katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe,watendaji wa vijiji,kata na wenyeviti wa vijiji wametakiwa kusimamia zoezi la kuwaondoa wakazi hao.
Aidha aliwataka wananchi kuwa waangarifu katika mlima huo na kutafakari madhara yatakayojitokeza ikiwa mlima huo watauharibu.
Alisesema wakazi watakaokaidi watafuatwa na mkuu wa Wilaya akiwa  na Askari ili kuwatoa kwa nguvu.
Awali katika ufunguzi wa maazimisho ya wiki ya maji duniani,serikali ya Mkoa wa Katavi ilisema kuwa itaendelea kulinda vyanzo vya maji vilivyopo Mkoani Katavi ikiwa ni sambamba na kutafuta namna ya kuendelea kutatua changamoto za baadhi ya wananchi hususani kukosa maji.
Hata hivyo baadhi ya wakazi katika Manispaa ya Mpanda walisema kuwa hawaoni haja ya kuwa na maadhimisho ya wiki ya maji ikiwa mwananchi anaendelea kukosa maji ya kunywa yaliyo safi na salama.
Maadhimisho ya Wiki ya maji duniani huanza kila mwka machi 16 ha kufikia kilele chake machi 22.

C.W.T YAWAMWAGIA MABATI WALIMU WASTAAFU MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald-Mpanda
CHAMA cha walimu C.W.T Mkoani Katavi kimekabidhi mabati 20 kwa walimu 11 wastaafu kutoka katika halamshauri za Nsimbo na Mpanda kwa kila mmoja kama sehemu ya kutambua mchango wao katika sekta ya elimu.
Akikabidhi mabati hayo Machi 24,2016,mjumbe wa kamati ya C.W.T taifa Bw.Costantine Marisel aliwataka walimu kuendelea kuzingatia maadili ya kazi yao.
Alisemakuwa miongoni mwa tabia zinazotakiwa kuepukika ni pamoja na walimu wa kiume kutofanya mapenzi na watoto wa kike,walimu wa kike kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike na walimu kuwachangisha fedha wanafunzi fedha ambazo hazitakiwi kuchangwa kwa kuwa kuna sera ya elimu bure.
Nao baadhi ya walimu waliopata msaada huo walikishukuru chama cha walimu CWT kwa kuwajali huku wakisema kuwa ni vizuri kuzingatia pia usafiri wao kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao.
Hatua hiyo pia ilipongezwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi wakisema kuwa hata taasisi nyingine zenye uwezo zifanye hivyo kwa ajili ya kuwasaidia kwa kuwa walitoa mchango mkubwa katika utumishi wao.

HARAMBE YAFANYIKA MPANDA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MADAWATI,MAHITAJI BADO LUKUKI
Na.Issack Gerald-Mpanda
Wadu mbalimbali wa elimu katika Manispaa ya Mpanda na halmashauri ya Wilaya ya Mpanda wamefanya harambee na kupata kiasi cha shilingi miloni 5 na elfu 65,madawati 224,mifuko 10 ya simenti na magogo 4 ya mbao kwea ajili ya kutengeneza madawati.
Machi 24,akizungumza wakati wa harambee hiyo,mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Pazza Tusamale Mwamlia aliwapongeza wadau hao kwa michango hiyo na kuwaomba kuendelea kuchangia kwa hiari.
Alisema kuwa Jamii haina budi kuendelea kujitolea kuchangia madawati kwani kila suala haliwezi kukamilika kwa kutegemea bajeti ya seriklai pekee.
Alisema kuwa changamoto ya madawati kumetokana na ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza ambapo kwa kiwango cha juu baadhi ya shule zimesajili wanafunzi hadi 800 kwa darasa la kwanza pekee.
Akisoma taarifa ya hali ya Mahitaji ya madawati katibu wa wa kamati ya kuratibu na kutengeneza madawati Bw.Lukasi Sotel Nyambala alisema kuwa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda ina upungufu wa madawati 8245 ambapo imetengenza madawati 1500 huku yanayohitajika kutengezwa yakiwa ni 7250 .
Kwa upande wa Manispaa ya Mpanda Bw.Nyambala alisema kuwa ina upungufu wa madawati 5179 ambapo yaliyotengenezwa ni  554 huku yanayohitajika kutengenezwa yakiwa 4625.
Serikali ya Tanzania ilisema matarajio ni ifikapo mwezi juni mwaka 2016 asiwepo mwanafunzi atakayekaa chini kwa kisingizio cha kukosa dawati la kukalia.

WAHITIMU MAFUNZO YA UHIFADHI HIFADHI ZA TAIFA WILAYANI KATAVI
Na.Agness Mnubi-Mlele
WAHITIMU wa Mafunzo ya Kujengwa uwezo wa uongozi katika uhifadhi wa hifadhi za taifa nchini wametakiwa Kujenga Mahusiano Mazuri na Jamii zinazozunguka hifadhi ili kuwawezesha  kupata taarifa za watu wanaojihusisha na matukio ya ujangili.
Kauli hiyo imetolewa na Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Katavi  Luteni Kanali Alex Ntazi Wakati wa  hafla ya Kufunga Mafunzo hayo iliyofanyika Katika Kituo cha Mafunzo Kilichopo Wilayani Mlele Mkoani hapa.
 Bw.Ntazi aliwataka wahitimu kuepuka vitendo vya rushwa,matumizi mabaya ya silaha,ulevi na utovu wa nidhamu na badala yake walinde rasilimali za taifa.
Aidha alisema wanatakiwa kuwa na mahusiano na watu wanaozunguka maeneo ya hifadhi ili kupatiwa taarifa sahihi za ujangili unaofanywa na waharibifu wa rasilimali za nchi.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa hifadhi za taifa Tanzania Bw.Ntango Mtaiko aliwataka wahitimu kuzingatia nidhamu ya kazi na kupamana na ujangili na kudumisha ushirikiano kati yao wenyewe na ndipo wahushe wengine.
Naye Mkurugenzi utumishi na utawala hifadhi za taifa tanapa Bi.Witness Shoo aliwataka wahitimu kufauata sheria,kanuni,taratibu na maelekezo katika kutekeleza majukumu.  
Awali akisoma taarifa ya kituo cha hifadhi cha mlele kaimu meneja mapori ya akiba Rukwa na Huhafwe Mark Chuwa aliiomba idara ya wanyama pori hifadhi za taiafa na Mkoa wa kuujumla kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho ikiwa ni pamoja na ufinuyu wa bajeti,upungufu wa vitendea kazi,mawasiliano na miundombinu.
Katika risala ya wahitumu iliyosomwa  na mmoja wa wahitimu Bi Angela Nyaki waliahidi kufanya kazi kwa weledi kwa kutumia mafunzo waliyoyapata.
Mafunzo hayo ya wahifadhi yaliyohitimishwa Machi 23,yaligawanyika katika makundi mawili amabpo kundi moja lilianza Februari 01 mwaka huu na kumalizika Februari 16 mwaka huu huku kundi la pili likianza Februari 22 na kuamlizika Machi 23 mwaka huu.

400 WABAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA KIFUAKIKUU KATAVI,IMANI ZA USHIRIKINA BADO KIKWAZO.
Na.Issack Gerald-Nsimbo
Machi 24 kila mwaka ni maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kifuakikuu duniani.Kupitia siku hiyo imegundulika kuwa  Zaidi ya wagonjwa 400 wamegundulika kuwa na maambukizi wa ugonjwa kipindupindu huku wagonjwa hao wakipatiwa matibabu na habari njema ikiwa ni kuwa hakuna mtu aliyefariki kutokona na ugonjwa huo.
Takwimu hiyo iliotolewa na mratibu wa kifuakikuu na ukoma Wilayani Nsimbo Mkoani Katavi Dk.Gabriel Kalumuna kwa niaba ya Daktari wa kikufua kikuu Mkoa wa Katavi ambapo amesema kuwa kati ya idadi ya wagonjwa hao hakuna kifo kichojitokeza na wote walipatiwa matibabu.
Alisema kuwa baadhi ya watu kuendelea kuwa na imani za kishirikina zinachangia kuendelea kuwepo kwa ugonjwa huo kwani watu huchelewa kupatiwa matibabu ambayo hata hakuna malipo yoyote.
Alisema kuwa vituo vinavyotoa huduma ya kupima kifuakikuu katika Wilaya ya Mpanda ni Hospitali ya Wilaya ya Mpanda,Kituo cha Afya Karema,Mwese na Mishamo huku vituo vyote vya afya vikitoa dawa kwa wagonjwa.
Miongoni mwa vituo visivyokuwa na uwezo wa kupima ni pamoja na Ilunde.
Aidha alisema kuwa idadi ya wagonjwa ni wanazidi idadi ya vituo vya afya ambapo aliiomba serikali kuviwezesha vituo vilivyoko mbali view na uwezo wa kupima wagonjwa hususani vijijini ambapo vijiji vingi vipo Halmshauri za Wilaya ya Mlele ,Mpanda Vijiji,Mpimbwe na Nsimbo.
Alisema kuwa ugonjwa huu husababishwa na aina ya vimelea vijulikanavyo kama MICROBACTERIA CHUBA  ambapo huenea kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mtu mwingine asiye na maambukizi kupitia hewa.
Kuna aina mbili za kifuakikuu cha mapafu ambazo hushambulia vioungo kama mifupa,figo,moyo na viungo vingine mwilini ambapo kwa habari nzuri ugonjwa huu hutibika ikiwa mgonjwa atawahi mapema kuanza matibabu.
Dalili za ugonjwa huu ni kukohoa kuanzia mwezi mmoja na kuendelea,kukosa hamu ya chakula,homa za mara kwa mara makohozi yaliyochanganyika na damu,kupungua uzito na kuhisi kifua kubanwa.
 Njia moja wapo ya kupambana na ugonjwa huu ni kujenga nyumba ambayo ina madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha na kuwahi mapema katika vituo vya afya kupatiwa matibabu.
Kwa takwimu ya Wizara ya Afya,watu wapatao 12000 hapa Tanzania hufariki dunia kutokana na ugonjwa huu.

RC RAPHAEL MUHUGA AITAKA WILAYA YA MLELE KUTORUHUSU MAGARI KUPITA DARAJA LA MTO KOGA
Na.Issack Gerald-Mlele
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Raphael Mugoya Muhuga aliuagiza uongozi wa serikali ya Wilaya ya Mlele kutoruhusu magari kupita katika daraja la mto Koga unaotenganisha Mkoa wa Katavi na Tabora.
Mkuu wa huyo wa Mkoa alitoa agizo hilo Machi 25 alipokuwa amefanya ziara Wilayani Mlele.
Alisema kuwa magari madogo yasiyo ya abiria ambayo yalikwishaanza kupita kutoka Mpanda Kuelekea Tabora yanaruhusiwa kupita isipokuwa magari makubwa ya abiria yataruhusiwa kupita mpaka daraja hilo likatapofunguliwa baada ya maji  kupungua.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mlele ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani humo Bw.Issa Suleiman Njiku alisema kuwa mto huo hupokea maji kutoka mito ya Rungwa na Chunya kupitia ziwa Rukwa huku akisema kuwa maisha yamepanda kwa wakazi wa wilaya hiyo kutokana na usafiri kudhorota.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Mlele Bw.Godwin Ben alisema kuwa tangu zuio liweke kwa magari kupita eneo hilo hakuna gari lililokuwa likipita ambapo alisisitiza kuwepo kwa usimamizi wa kutosha.
Mtalaamu wa wakala wa barabara Tanroads kutoka makao makuu ya Mkoa wa Katavi alisema kuna haja ya kufanya ukaguzi wa kina kuhakikisha usalama wa daraja unakuwepo muda wote.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa alitoa rai kwa mkandarasi aliyepewa tenda ya kujenga daraja hilo kuanza matengenezo ya daraja hilo haraka iwezekanavyo huku akisema kuwa kinachotakiwa ni kuangalia namna ya kuongeza bidhaa mjini Inyonga kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu waishio mlele.
Daraja la Mto Koga lilikatika Januari 26 mwaka 2016 na kupelekea vifo vya watu 10 baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji.
Asante kwa kuchagua P5 TANZANIA MEDIA,ukiwa na maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com na endelea kufuatilia habari katika blog hii kwa kuandika P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA