ZAIDI YA WALIMU 3 WAFUNDISHA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU KATIKA UBAO MMOJA,DARASA MOJA WAKATI MMOJA MANISPAA YA MPANDA


Na.Issack Gerald-Mpanda
ZAIDI ya walimu watatu wamekuwa wakifundisha wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Azimio katika darasa moja na ubao mmoja kwa darasa la kwanza hadi la saba kwa miaka saba sasa.

Hayo yamebainishwa na walimu wa shule ya Msingi Azimio akiwemo mwalimu mkuu wa Shule hiyo Mwl.Beno Mahema ambapo imebainika kuwa miongoni mwa chanzo cha hali hiyo ni Mkandarasi kufunga madarasa akishinikiza kulipwa zaidi ya milioni 28 anazodai.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni amekiri kuwepo hali hiyo na amesema kuwa Alhamisi ya Februari 4 mwaka huu wanatarajia kufanya mazungumzo baina ya uongozi wa Manispaa na Mkandarasi ili pesa inayodaiwa Manispaa zilipwe na madarasa yaruhusiwe kutumiwa na wanafunzi.
Mpaka sasa kuna Jumla ya Wanafunzi wenye ulemavu 18,walimu 4 ambapo hata hivyo katika mpango wa Rais wa elimu bure wametengewa shilingi laki tatu kwa ajiri ya chakula.
Kwa upande wake Mkandarasai wa Kampuni ya Mwandoya Investment Bw.Paul Luguyashi ameendelea kusemakuwa hataruhusu madarasa yatumiwe na wanafunzi mpaka atakapopewa malipo yake ya zaidi ya Shilingi milioni 28 kwa sasa.
Kwa mjibu wa Mkataba wa makubaliano,mkandarasi huyu ilitakiwa alipwe shilingi milioni 32 kama sehemu ya mkataba wote baada ya kukamilisha ujenzi wa majengo mwezi Aprili mwaka 2014 baada ya kupewa tenda hiyo mwaka 2013.
Kwa hiyo kutokana na malimbikizo ya deni la Shilingi milioni 5 kutoka mwaka 2014,ilizidi kuongezeka pamoja na riba yake kutoka milioni 5 hadi kufikia zaidi ya Shilingi milioni 28 anazodai hadi sasa.
Hata hivyo Bw.Lunguya ameendelea kusisitiza kuwa katu hatofungua madarasa hayo ikiwa hatalipwa pesa yake anayodai.
Katika hatua nyingine,wazazi wenye watoto wenye ulemavu Mkoani Katavi wametakiwa kuwapeleka shuleni ili wakapate haki yao ya elimu kama walivyo watoto ambao siyo walemavu.
Wanafunzi walemavu walipo katika shule ya msingi Azimio ni wasioona,wasiosikia,wenye ulemavu wa akili na viungo ambpo kwa Mkoa wa Katavi zipo shule karibu tano zenye watoto wenye mahitaji maalumu ambapo kwa Manispaa ya Mpanda mbali na Azimio shuleni nyingine ni Shule ya Msingi Nyerere yenye wanafunzi wenye mtindio wa ubongo.
Hata hivyo wanafunzi wote wawili waliofanya mtihani mwaka 2015 walifaulu kwa daraja B na C na kuwa miongoni mwa wanafunzi waliosababisha Manispaa ya Mpanda kuongoza kwa miaka miwili mfululizo kitaifa katika matokeo ya darasa la saba.
Mshirikishe mwenzako kasha toa maoni yako mdau wangu kupitia hapahapa P5 TANZANIA MEDIA au geraldissack@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA