WABUNGE VITI MAALUM MPANDA WATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA,WATOA MSAADA WAAHIDI MAKUBWA.


Na.Meshack Ngumba-Mpanda
SERIKALI imeshauriwa kufanyia kazi changamoto zilizopo katika hospitali ya wilaya ya Mpanda ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za afya.

Ushauri huo umetolewa na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Bw. Naibu Mkongwa wakati akizungumza na wabunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi Bi. Taska Mbogo na Bi. Anna Lupembe walipotembelea hospitalini hapo.
Kwa Upande wao wabunge hao wameahidi kushirikiana na uongozi wa hospitali, kwa kutoa misaada itakayosaidia kupunguza kero ndogo ndogo kwa wagonjwa.
Katika ziara hiyo pia wabunge hao wametembelea wodi mbalimbali za wagonjwa na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni za  kufulia.  
Katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda,kumekuwepochangamoto lukuki zikiwemo uhaba wa dawa,hali tete ya usafi,wauguzi kutumia lugha isiyo na ustaarabu kwa wagonjwa na uhaba wa vitanda hali inayosababisha wagonjwa wawili kulala kitanda komoja.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA