SILAHA 4 ZAKAMATWA KATAVI ZIPO MBILI ZA KIVITA WAMILIKI WAKE WATELEKEZA PIA PIKIPIKI WATOKOMEA KUSIKOJULIKANA WENYE GOBOLE WAO WADAKWA NA POLISI.


Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la polisi Mkoani Katavi,limekamata silaha nne zikiwemo silaha mbili za kivita aina ya SMG na pikipiki moja aina ya Huoniao yenye namba za usajili T.948BHU za watu wanaosadikika kuwa ni majambazi.
                                               
Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavoi ACP Rashid Mohamed akiwa ameshika silaha aina ya SMG za kivita zilizokamatwa kwa watuhumiwa wakiwa katika harakati za kufanya uharifu.(PICHA NA.Issack Gerald Februari 26,2016)


Watuhumiwa waliokamtwa na silaha mbili aina ya gobole(PICHA NA.Issack Gerald Februari 26,2016)

Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed akionesha miongoni mwa silaha ambazo zimekamatwa(PICHA NA.Issack Gerald Februari 26,2016)

Katika picha ni Silaha aina ya SMG ambazo ni za kivita zikiwa ni miongoni mwa silaha 4 ambazo zimekamatwa (PICHA NA.Issack Gerald Februari 26,2016)

Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed amesema,silaha hizo aina ya SMG zenye namba AE 352720 na UA 3879 zenye risasi 62,zilkamatwa jana Februari 25 majira ya saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Kasekese Kata ya Sibwesa Wilayani Mpanda zikiwa na magazine mbili.
ACP Mohamed alisema kuwa majambazi hayo yalipokutana na askari wa doria yakiwa na pikipiki hiyo yenye rangi nyekundi wakiwa na silaha hizo hawakutaka kusimama waliposimamishwa na Polisi hao ambapo walitelekeza pikpiki  na hatimaye kutokomea kusikojulikana ambapo baada ya upekuzi kufanyika ndipo zilipokutwa silaha hizo mbili za kivita aina ya SMG zikiwa na magazine mbili zikiwa zimeviringishwa ndani ya suruali ya Jinsi na kufungwa kwenye tenga nyuma ya pikipiki.
Wakati huo huo ACP Mohamed amewataja watu wawili waliokamatwa Februari 24 majira ya usiku wakiwa na silaha aina ya Gobole kuwa ni Donath Laurent(32) mkazi wa Nkungwi aliyekamatwa na silaha moja aina ya gobole huku silaha hiyo ikiwa imefichwa kwa kuhifadhiwa kwenye majani nje ya nyumba yake ambapo kwa upande wa Bw. Geofrey John Pandisha(34) mkazi wa Nkungwi naye akikamatwa akiwa na silaha moja aina ya gobole akiwa nayo shambani kwa ajili ya kuwinda wanyamapori ambapo wote ni wakazi wa kata ya Sibwesa Wilayani Mpanda.
Watuhumiwa walikamatwa wanatarajia kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika huku likiendelea kuwasaka watuhumiwa wa ujambazi.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ametoa rai kwa wananchi wanaomiliki silaha ki nyume na utaratibu na kutaka wasisalimishe silaha hizo mara moja ili kuepuka mkono wa sheria dhidi ya wahusika wenye silaha kama hizo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA