MZIMU WA RUSHWA WAENDELEA KUWATESA POLISI KATAVI,ASKARI WA JESHI LA POLISI MWINGINE MBARONI KATAVI KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA


Na.Issack Gerald-Katavi
Askari wa jeshi la polisi Mkoani Katavi PC.G.451 Peter Exavery ameshitakiwa katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma ya kupokea rushwa ya shilingi laki moja (100,000=/) kutoka kwa mzee aliyefahamika kwa jina la Ruchege Mambalo ili kumfutia tuhuma ya mkumjeruhi mtoto wake Lutobhisha Mambalo.
                                                  

Akito taarifa kwa vyombo vya habari,wakili na mwendesha mashtaka wa Takukuru Mkoani Katavi Bw.Bahati Stafu Haule,amesema kuwa tukio la askari wa jeshi la polisi Bw. Peter Exavery Kashuta kushawishi kuomba na kupokea rushwa,lilitokea mnamo Februari 09 katika Kitongoji cha Lwega kwenye mgahawa wa Lwega,kijiji cha Lwega Namba 7A,Kata ya Mwese  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Vijijini.
Bw. Haule amesema kuwa,Manamo Februari 10,2016,Tume ya kupambana na kuzuia Rushwa Takukuru Mkoani Katavi lipokea taarifa kutoka kwa Ruchege Mambalo aliyewekwa mahabusu katika kituo kidogo cha polisi Mwese Februari 09,2016 kwa tuhuma ya kumpiga mtoto waked Lutobhisha Mbambalo amabaye ana matatizo ya ya akili alipotaka kumchoma kisu baba yake ambapo katika harakati za kujiokoa,Luchege mambalo alichukua jiwe na kumpiga mtoto huo usoni ambapo mtoto huyo alikimbilia haraka kituo cha pilisi Mwese kutoa taarifa.
Amesema kuwa wakati Bw.Mambalo akimtafuta mtoto wake ali mkuta mtoto huyoakiwa na askari Peter Exavery Kashuta ambapo baada ya mzazi wa mtoto huyo kufika askari huyo alishawishi mzee huyo kupewa laki saba (700,000/= ili amwachie huru na kumfutia tuhuma ya kujeruhi.
Aidha,Bw. Haule alifafanua kuwa baada ya taratibu za jeshi la polisi kukamilika Februari 17,2016,mtuhumiwa alifikishwa mahakamani katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Mh.Chiganga Tengwa hakimu mfawidhi mkazi wa Wilaya na kufunguliwa kesi ya jinai Namba.61/02/2016 na kusomewa mashtaka mawili ambayo ni Kuomba au kushawishi rushwa ya shilingi laki saba(700,000/=) huku shtaka la pili likiwa ni kupokea rushwa ya shilingi laki moja (100,000) jambo ambalo lilikuwa na kinyume au matakwa ya mwajiri wake kwa mjibu wa kifungu 15(1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa na 11/2007.
Hata hivyo aliachiwa kwa dhamana ya kukidhi matakwa ya dhamana alizoweka mahakamani hapo ambazo ni mdhamini mmoja mwenye hati ya au dhamana ya fedha taslimu milioni bili(2,000.000/=) na kutosafiri nje ya Mkoa wa Katavi bila kibali cha Mahakama ya Wilaya.
Aidha,Takukuru Mkoani Katavi imetoa angalizo na wananchi na watumishi wote wa umma kujiepusha na vitendo vya rushwa huku jeshi la polisi likitakiwa kutambua kulinda usalama wa raia ikiwa ni pamoja na fedha.
Februari 16 mwaka huu,Mwanasheria Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Falhati Seif Khatibu na askari magereza wawili wa gereza la mahabusu Mpanda walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa wa mauaji ya mlemavu wa ngozi albino.
Vitendo hivi mpaka lini?toa maoni kwa facebook ni Issack Gerald,Sauti Ya Katavi na Blog P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Asante kwa kuendelea kuchagu P5 TANZANIA MEDIA,Mshirikishe na mwenzio.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA