MTANDAO WA RADIO ZA JAMII (COMNETA) WAZUNGUMZIA SIKU YA RADIO DUNIANI INAYOFANYIKA FEBRUARI 13,KILA MWAKA.



Na.Issack Gerald-Katavi
Mtandao wa Radio za Jamii Tanzania (COMNETA) umetoa rai kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya seriklai za mitaa mpaka ngazi ya taifa,kutumia radio mara kwa mara kwa lengo la kuelimisha na kufikisha ujumbe katika jamii kuliko kiongozi kutumia radio kwa wakati Fulani kwa maslahi binafsi.
                                         
Mwenyekiti wa Radio za kijamii Bw.Joseph Sekiku hivi karibuni (Aliyesimama) akizungmzia masuala yanayohusu radio za kijamii Jijini Dar es Salaam

Rai hiyo imetolewa leo na viongozi wa mtandao huo Tanzania na umoja wa Mataifa,wakati wa mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kuhusu siku ya radio duniani ambayo inatarajia kuadhimishwa kesho duniani kote.
Katika mahojiano hayo, Mwenyekiti wa Mtandao huo Bw.Joseph Sekiku amesema kuwa redio za jamii Tanzania zimesaidia katika utatuzi wa migogoro baina ya wakulima na wafugaji  kwa kuelimisha jamii matumizi bora ya ardhi pamoja na kuunganisha watawala na watawaliwa kwa lengo la kudumisha amani na kutatu migogoro hiyo kwa mazungumzo.
Amewaasa viongozi wa umma katumia vyombo mbalimbali vya habari za kijamii kufikisha ujumbe kwa kuwa radio zipo kwa ajili kuelimisha,kuburudisha,kuasa na kuhabarisha.
Kwa upande wake Meneja wa Mpanda Radio Fm ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa  mtandao wa Radio  za jamii (COMNETA) Bw.Prosper Laurent Kwigize amesema kuwa vyuo mbalimbali vinavyoendesha mafunzo ya uandishi,utangazaji na taaluma yote ya habari kwa ujumla,vinatakiwa kuwa na wakufunzi wenye weledi wa taaluma ya habari  ili kupata watalaamu wa taaluma hiyo wenye uwezo wa kusaidia jamii na kuepuka kuendelea kuwa wanafunzi wanapopata kazi katika taasisi.
Aidha Bw.Prosper amesema kuwa wanasiasa wanatakiwa kutambua umuhimu wa radio hata baada ya kampeni za uchaguzi kufanyika kuliko kutambua vyombo vya habari wakati wa kampeni za kusaka kura pekee na baada ya hapo kutorejea kuzungumza na waliompigia kura ili watambue ni kitu gani kinachoendelea katika kushughulikia ahadi zake.
                                              
Meneja wa Mpanda RADIO na makamu mwenyekiti wa Mtandao wa jamii Radio Tanzania Bw.Prosper Laurent Kwigize (Picha na Issack Gerald)
Katika mahojiano hayo,Bi.Stela Vuzo ambaye ni Afisa Habari kutoka umoja wa Mataifa aliyeko hapa nchini mbali na kuvitaka vyombo vya habari kufuata miongozo ya vyomvo vya habari kuepuka uvunjifu wa amani nchini.
Wakati huo huo,amewataka wanawake na vijana kutumia vyombo vya habari ikiwemo radio kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili na masuala ya kijasiliamali.
Kwa mjibu wa Shirika la kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limesema kuwa jumla ya watu milioni 20 duniani Kote wanasikiliza na kutegemea radio katika kuzungumzia masuala mbalimbali ya kijamii.
Maadhimisho ya siku ya Radio Duniani huadhimishwa ila mwaka ifikapo Februari 13,ambapo kwa mara ya kwanza maadhimisho haya yalifanyika mwaka 1946 kote duniani.
Kauli mbiu ya siku ya Radio Duniani “REDIO  KAMA CHOMBO CHA HABARI WAKATI WA MAJANGA”.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA