MKUU WA WILAYA YA MLELE ATOA SIKU 4 KWA MAAFISA HALMASHAURI ZA WILAYA ZA NSIMBO,MPIMBWE NA MLELE WAWE WAMEKABIDHI TAARIFA YA MADAWATI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI


Na. Agness Mnubi-Nsimbo
MAAFISA tarafa,Watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri za Nsimbo,Mlele na Mpimbwe wamepewa siku 4 za kutembelea shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Halmashauri zao ili kubaini upungufu wa madawati.

Agizo hilo limetolewa jana na  Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu Issa Suleiman Njiku katika kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Mlele kilichofanyika katika Halmashauri ya Nsimbo,na kuwataka ifikapo February 12 kutoa taarifa za upungufu wa madawati.
Amesema wanatakiwa kushirikiana ili kuzunguka katika shule za sekondari na msingi  kufahamu idadi ya madawati yaliyopo na pungufu .
Amesema ifikapo february 28 Halamashauri hizo zinatakiwa kuwa zimetatua changamoto ya upungufu wa madawati, huku Mkoa ukizitaka Halmashauri zote kutataua tatizo hilo ifikapo mwishoni mwa   mwezi machi mwaka huu.
Halmashauri zote nchini zinatakiwa  kutekeleza agizo la Serikali kuwa hakuna mwanafuzi anayetakiwa kukaa chini ifikapo juni 30.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA