MATUKIO YA WIKI NDANI NA NJE YA KATAVI KUANZIA FEBRUARI 15—20,2016.


MATUKIO YA WIKI NDANI NA NJE YA KATAVI KUANZIA FEBRUARI 15—20,2016.
Wednesday, 17 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, February 17, 2016
                                                                                                             



Na.Issack Gerald-Katavi
Watu watano akiwemo Mwanasheria Mkuu Mkoani Katavi Bw. Falhati Seif  Khatibu (45),wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa  Alex Manyanza Enock (27) Mkazi wa majimoto aliyekuwa anakabiliwa na kesi NA. MTO/IR/76/2015 ya kujaribu kuua mlemavu wa Ngozi Albino Limi Luchoma(30) mkazi wa kijiji cha Mawiti kata ya Majimoto Wilayani Mlele.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Rashid Mohamed,amewataja watuhumiwa kwa ujumla kuwa ni A. 287 Sajenti John Musa (50) mkazi wa mtaa wa mji mwema Wilayani Mpanda, A. 5385 Sajenti Deogartius Katani (50) Mkazi wa mtaa wa Kigamboni Wilaya ya Mpanda wa gereza la mahabusu Mpanda.
Kamanda pia amewataja wengine wanaotuhumiwa kuwa ni Mwanasheria mkuu wa Mkoa wa Katavi   Falhati Seif  Khatibu (45) mkazi wa maeneo ya Msakila Shule ya Msingi ,Masanja Kasinje Kasala(33) mkazi wa Kakese Mkwajuni Wilayani Mpanda pamoja na Ngassa Mashindike (37) mkazi wa Majimoto Wiayani Mlele.
Kamanda Mohamed amesema kuwa mnamo 19.01.2016 majira ya saa 09:30 asubuhi,Jeshi la Polisi Mkoani Katavi lilipokea taarifa toka kwa raia wema kuwa mtuhumiwa  Alex Manyanza Enock hayupo gereza la mahabusu Mpanda.
Baada ya taarifa hizo kupokelewa,jeshi la polisi lilianza upelelezi na kubaini kuwa mtuhumiwa huyo alitoroka tangu tarehe 12.10.2015 katika gereza la mahabusu Mpanda ambapo awali mtuhumiwa huyo aliwahi kutoroka akitumikia kifungo cha miaka 5 kwa kosa la wizi wa mifugo katika gereza la kilimo la Kalilankulukulu kabla ya kukamatwa kwa kesi hii ya kujaribu kuua.
Kamanda ameendelea kufafanua kuwa,ilipofika 21.01.2016 wakati jeshi la polisi likiendelea na upelelezi wa kesi hiyo,zilipokelewa taarifa za kuwa mtuhumiwa Alex Manyanza Enock anapatikana Mkoani Rukwa ambapobaada ya ufuatiliaji,mtuhumiwa alipatikana akiwa amejificha katika kijiji cha Kipande Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.
Katika mahojiano ya kina,mtuhumiwa Bw. Alex Manyanza Enock alieleza jinsi alivyofanikishiwa mipango ya kutoroka gerezani akimtaja mjomba wake Bw.Masanja Kasinje Kasala pamoja na rafiki yake Ngassa Mashindike ambao naobaada ya kukamatwa walikiri kufanya mipango ya kumtorosha mtuhumiwa kwa lengo la kuwafanya watuhumiwa wengine katika kesi yao ya kujaribu kuua kutotiwa hatianki akiwemo mjomba wake walioko pamoja katika kesi hiyo Bw.Masunga Kashinje.
Mtuhumiwa alieleza kuwa waliwashirikisha askari magereza wawili ambao ni A. 287 Sajenti John Musa Masagula na  A. 5385 Sajenti Deogratius Katani wote wakazi wa kituo cha kazi gereza la mahabusu Mpanda ambao walipatiwa  kiasi cha Shilingi  milioni moja(1,000,000/= ) ili kumwezesha mtuhumiwa kutoroka.
Pia walimtaja mwanasheria mkuu wa serikali ya Mkoa wa Katavi Bw. Falhati Seif  Khatibu  ambapo walidai walimpatia kiasi cha shilingi milioni mbili (2,000,000/=)ili kumwondolea shitaka mtumiwa Masunga Kashinje baada ya kuwa mtuhumiwa Alex Manyanza Enock amefanikiwa kutoroka.
Hata hivyo,Kamanda wa polisi Mkoani Katavi ametoa wito kwa watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi kufanya kazi kwa kufuata misingi ya utumishi huku wakiendelea kuihudumia jamii kwa ukaribu.

Wednesday, 17 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, February 17, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda
Watumishi wa umma Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wametakiwa kutofanya kazi kwa nidhamu ya woga na badala yake watumie taaaluma waliyoisomea.
Wito huo umetolewa Siku ya Jumanne Februari 17 na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima kikao cha kamati ya ushauri ambacho kimefanyika kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kikao ambacho kimefanyika jana katika ukumbi wa iadara ya maji Mjini Mpanda.
Kikao hicho ambacho kimefanyika ukmbi wa idara ya maji kinawahusisha viongozi na wakuu wa idara mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi ngazi ya Wilaya na Mkoa.
Akiwasilisha taarifa katika kikoa hicho cha kupitisha mpangao wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017,Mchumi wa Manispaa ya Mpanda Bi.Mary Kanumba,katika taarifa yake ameiomba serikali kuidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 23.8. kwa ajili ya kuekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na shughuli nyingine za kiutawala na maendeleo.
Amesema kuwa,Shilingi Bil.19.3 ni kwa ajili kwa bajeti ya kawaida na Shilingi Bil.4.4 nje ya komo wa bajeti.
Bi.Kanumba Mapato ya ndani katika Manispaa,amesema kuwa pato limeongezeka kutoka Shilingi Bil.1.9 hadi Shilingi Bil.2.3 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 18.5 ambapo ongezeko hilo limechangiwa na vyanzo mbalimbali vya mapato vikiwemo  kodi ya majengo,ushuru wa zao la tumbaku,leseni za biashara,minada na ushuru wa vileo.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017,katika taarifa ambayo imesomwa na Mchumi wa Halmshauri ya hiyo Bw.Filemon Mrageri,Halmshauri ya Mpanda imeomba kuidhinishiwa Shilingi Bilioni Bil 31 Mil.584 laki moja thelathini na sita elfu mia saba na arobaini (31,584,136,740) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.
Hata hivyo,bajeti ya malipo ya mishahara ya wafanyakazi imeonekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa miongoni mwa sababu ikiwa ni utanuzi wa mipaka ya utawala na ajira mpya kwa watumishi katika Halmashauri zote za Manispaa ya Wilaya ya Mpanda.
Kikao hicho muhimu katika Halimashauri,kimeshirikisha Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao,wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara mbalimbali katika katika halimshauri zote,watendaji wa kata na baadhi ya viongozi kutoka Idara katika ngazi ya Mkoa akiwemo Meneja wa Idara ya Maji Mpanda Injinia Zacharia Nyanda na Meneja Mpya wa wa Kwanza wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Katavi. 

TAMKO LA IDARA YA MAJI KATAVI KUPITIA KIKAO CHA TAREHE 16 FEBRUARI CHA KUPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2016/2017                                      


Na.Issack Gerald-Katavi
Idara ya Maji Mkoani Katavi ilisema kuwa mradi wa Orestria unaoshughulikia ukarababti na ujenzi wa mambomba na vyanzo vya maji unaotarajia kuanza mwezi ujao,kutawaondolea wananchi adha ya kukosekana kwa maji na hivyo maji kupatikana kwa saa 24 katika mji wa Mpanda.
Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Maji Mkoa wa Katavi Injinia Zzacharia Nyanda wakati akijibu hoja za wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri cha kupitisha mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa idara ya maji.
Amesema kuwa mradi huo pamoja na kuweka mabomba mapya ya kupitisha maji,mradi huo unataraji kujenga chanzo cha Maji Ikorongo Na.2 ili kupata tenki lenye ujazo wa lita milioni moja huku tenki linguine likjengwa vijijini.
Hata hivyo Injinia Nyanda amesema kuwa ikiwa mradi wa Oretria hautakuwepo,Shilingi milioni 7 zitahitajika ili kuondoa  kabisa tatizo la mgao wa maji katika Manispaa ya Mpanda.
Aidha amesema kuwa tatizo linguine linalopelekea maji kukosekana kwa kiwango kikubwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi hususani Manispaa ya Mpanda ni kunatokana na kiasi kidogo cha uzalishaji wa maji katika Manispaa ya Mpanda,mabomba yenye upana mdogo tena ya chuma,mabomba kuziba na mengine kukatika kutokana na mabomba hayo kuwa ya muda mrefu.
Amesema kuwa kiwango cha maji kinachozalishwa ni lita mil.3,360,000 huku mahitaji yakiwa ni lita mil.9,500,000 ambapo kwa kiwango hicho ni sawa na upungufu wa lita mil.6,140,000.
Bw.Nyanda alitoa ufafanuzi zaidi wa mradi unaotaraji kuanza mwezi machi mwaka huu.
Baadhi ya mitaa ya kilimahewa,Kawajense ,Rungwe,Nsemulwa migazini,Aitel na Ilembo hazina matatizo makubwa ya ukosefu wa maji huku Kata ya Makanyagio na Mpanda Hotel zikiongoza kwa kuwa na mabomba yaliyoziba mabomba yenye upana mdogo na kukumbwa na mgao wa maji mara kwa mara.

TAARIFA YA UFAFANUZI WA MATMIZI YA MITI KATIKA MATUMIZI MBALIMBALI KUPITIA KIKOA CHA KUPITISHA BAJETI.
Afisa misitu Wilaya ya Mpanda Bw.Lucas Nyambala alitoa ufafanuzi wa matumizi ya miti ya kupandwa na isiyo ya kupandwa ambapo miti mingi imekuwa ikitumika kwa matumizi ya uchanaji mbao,kuni,uchomaji mkaa na matumizi mengine.
                      
 Wednesday, 17 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, February 17, 2016

Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
WANAFUNZI wa Shule za Sekondari katika Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani katavi wametakiwa kusoma masomo ya sayansi.

Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Michael Nzyungu wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda redio,akisema kuwa wanafunzi wajitokeze kwa wingi kusoma masomo ya sayansi ili kufaidi maabara zilizopo katika shule za sekondari za Halmashauri ya Nsimbo.
Amesema Lengo la Serikali kujenga maabara kila shule ya sekondari ni kuinua kiwango cha elimu kwa masomo ya sayansi hivyo wanafunzi hawana budi kusoma masomo ya sayansi ili kutumia maabara hizo.
Amesema wanazidi kuboresha maabara hizo kwa kuhakikisha kuwa na  miundombinu mizuri, kuongeza  vifaa vya kutosha na walimu wa masomo ya sayansi.
Kauli ya mkurugenzi mtendaji huyo inakuja ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa lengo la kupata wataalamu katika masuala mbalimbali hapa nchini.
Hata hivyo licha ya hamasa hiyo,kunahitajika walimu zaidi wa masomo ya sayansi wenye uwezo thabiti.

 

Thursday, 18 February 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, February 18, 2016

Na.Issack Gerald-Katavi
Agizo la naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi  Mh.Willium Tate Ole Nashe la kumtaka mrajisi vya vyama vya  ushirika hapa nchini kuteua  timu ya kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku wa Chama cha Ushirika Mpanda Kati wanaolalamika kutolipwa madai yao karibu milio 600 halijatekelezwa.

Akizungumza na Mpanda Radio fm Ofisini kwake,Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Katavi Bw.Luhiguza Medadi Sesemukwa amesema kuwa,taarifa iliyopo kutoka kwa mrajisi  ngazi ya taifa aliyeagizwa kufanya ukaguzi  huo amesema timu hiyo imechelewa kufika kutekeleza agizo la waziri kutokana na ukosefu wa fedha.
Bw.Sesemukwa amesema kuwa,wajumbe wa timu kutoka tume ya maendeleo ya ushirika  iliyoundwa na mrajisi wa vyama vya ushirika nchini inatarajia kufika Mkoani Katavi wakati wowote kuanzia leo.
Hata hivyo shirika la wakaguzi wa vyama vya ushirika COWASCO kutoka Mkoani Tabora kwa sasa wapo Mkoani Katavi kuanzia Februari 14 mwaka huu na wanaendelea ukaguzi wa madai ya wakulima.
Amesema mara baada ya timu kutoka Dodoma ambako ndiko makao makuu yao yaliko,wataungana na timu timu iliyotoka Tabora kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi na uchunguzi wa kina.
Agizo la naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi  Mh.Willium Tate Ole Nashe la kumtaka mrajisi vya vyama vya  ushirika hapa nchini kuteua  timu ya kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku wa Chama cha Ushirika Mpanda Katavi wanaolalamika kupokonywa mamilioni hayo ya fedha,lilitolewa Januari 11,mwaka huu akitoka agizo la kuundwa na kutumwa timu ya ukaguzi ndani ya siku 14 kuanzia siku ya agizo kutolewa.
Katika hatua nyingine amewataka wakulima waliotoa hoja ya madai yao kutuo uthibitisho wa vielelezo ili kubaini ukweli wa malalamiko.
Mbali na malalamiko ya kutoripwa kitita hicho karibu miloni 600,pia walilalamikia  kulipwa kwa thamani ya dola badala ya shilingi,kuuziwa pembejeo kwa bei kubwa na kulipa kwa dola na kutokuona msaada wa Chama kikuu cha ushirika LATCU kwa wakulima wa zao la tumabku badal aya kuwanyonya.
Wakati huo huo,amewashauri Mrajisi Sesemukwa ametoa rai kwa wakulima kuendelea kupanda miti,kutumia Mabani ya kisasa ya kuchomea tumbaku yanayotumia kuni kidogo kwa ajili ya kuhifadhi mazingira.
Lakini pia amewataka wakulima kutotorosha tumbaku na kwenda kuuzia nje ya kampuni iliyoidhinishwa kununua tumbaku yake ili kuepuka kusababisha mlundikano wa madeni watakayodaiwa.
Majibu ya mrajisi wa Mkoa,yanakuja kufuatia malalamiko ya wakulima kuanza kujitokeza wakilalamika kutokuona agizo la waziri kutotekelezeka.

 Friday, 19 February 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Friday, February 19, 2016

Na.Issack Gerald-Katavi
Askari wa jeshi la polisi Mkoani Katavi PC.G.451 Peter Exavery ameshitakiwa katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma ya kupokea rushwa ya shilingi laki moja (100,000=/) kutoka kwa mzee aliyefahamika kwa jina la Ruchege Mambalo ili kumfutia tuhuma ya mkumjeruhi mtoto wake Lutobhisha Mambalo.
Akito taarifa kwa vyombo vya habari,wakili na mwendesha mashtaka wa Takukuru Mkoani Katavi Bw.Bahati Stafu Haule,amesema kuwa tukio la askari wa jeshi la polisi Bw. Peter Exavery Kashuta kushawishi kuomba na kupokea rushwa,lilitokea mnamo Februari 09 katika Kitongoji cha Lwega kwenye mgahawa wa Lwega,kijiji cha Lwega Namba 7A,Kata ya Mwese  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Vijijini.
Bw. Haule amesema kuwa,Manamo Februari 10,2016,Tume ya kupambana na kuzuia Rushwa Takukuru Mkoani Katavi lipokea taarifa kutoka kwa Ruchege Mambalo aliyewekwa mahabusu katika kituo kidogo cha polisi Mwese Februari 09,2016 kwa tuhuma ya kumpiga mtoto waked Lutobhisha Mbambalo amabaye ana matatizo ya ya akili alipotaka kumchoma kisu baba yake ambapo katika harakati za kujiokoa,Luchege mambalo alichukua jiwe na kumpiga mtoto huo usoni ambapo mtoto huyo alikimbilia haraka kituo cha pilisi Mwese kutoa taarifa.
Amesema kuwa wakati Bw.Mambalo akimtafuta mtoto wake ali mkuta mtoto huyoakiwa na askari Peter Exavery Kashuta ambapo baada ya mzazi wa mtoto huyo kufika askari huyo alishawishi mzee huyo kupewa laki saba (700,000/= ili amwachie huru na kumfutia tuhuma ya kujeruhi.
Aidha,Bw. Haule alifafanua kuwa baada ya taratibu za jeshi la polisi kukamilika Februari 17,2016,mtuhumiwa alifikishwa mahakamani katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Mh.Chiganga Tengwa hakimu mfawidhi mkazi wa Wilaya na kufunguliwa kesi ya jinai Namba.61/02/2016 na kusomewa mashtaka mawili ambayo ni Kuomba au kushawishi rushwa ya shilingi laki saba(700,000/=) huku shtaka la pili likiwa ni kupokea rushwa ya shilingi laki moja (100,000) jambo ambalo lilikuwa na kinyume au matakwa ya mwajiri wake kwa mjibu wa kifungu 15(1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa na 11/2007.
Hata hivyo aliachiwa kwa dhamana ya kukidhi matakwa ya dhamana alizoweka mahakamani hapo ambazo ni mdhamini mmoja mwenye hati ya au dhamana ya fedha taslimu milioni bili(2,000.000/=) na kutosafiri nje ya Mkoa wa Katavi bila kibali cha Mahakama ya Wilaya.
Aidha,Takukuru Mkoani Katavi imetoa angalizo na wananchi na watumishi wote wa umma kujiepusha na vitendo vya rushwa huku jeshi la polisi likitakiwa kutambua kulinda usalama wa raia ikiwa ni pamoja na fedha.
Februari 16 mwaka huu,Mwanasheria Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Falhati Seif Khatibu na askari magereza wawili wa gereza la mahabusu Mpanda walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa wa mauaji ya mlemavu wa ngozi albino.
Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena machi 17 mwaka huu itakaposikilizwa.
RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA WATANZANIA KUPITIA WAZEE WA DAR ES SALAAM HOTUBA YAGUSA MAENEO YOTE.
Rais Dk John Pombe Magufuli Februari 13,2016 alilihutubia taifa kupitia wa Wazee wa Dar e salaam ambapo ameainisha changamoto kadhaa zinazolikabili taifa na mikakati inayochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano kuikabili.
Akizungumza na wazee hao wa Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo, Rais Dk John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali ya awamu ya tano anayoingoza imejipanga vyema kuwatumikia na kukabili matatizo yao.
Katika hotuba yako hiyo iliyochukua takriban saa moja na kugusa maeneo yote muhimu, Rais ametahadharisha viongozi na wananchi wengine kuhusu ubadhirifu wa mali ya umma.
Aidha, Rais Dk John Pombe Magufuli amezungumzia kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar ambapo amesema yeye kama Rais ni vigumu kuingilia maamuzi ya tume ya taifa uchaguzi Zanzibar ambayo ni huru.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es saalam alizungumzia changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wa Dar es salaa hususan katika utekelezaji wa agizo la utoaji wa elimu bure.
Katika hatua nyingine,Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kutumbua majipu kwa watu waliokabidhiwa madaraka halafu hawawajibiki ipasavyo na badala yake kuendekeza ufisadi na kuharibu mali ya umma.

Friday, 19 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, February 19, 2016

Na.Mwandihi wetu-Dar es Salaam
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu amewataka Makamanda wa Polisi kote nchini kuendesha oparesheni kali ya kuwachukulia hatua kali za kisheria waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani ikiwemo kubeba abiria zaidi ya mmoja, kupita katika taa nyekundu pamoja na kutovaa kofia ngumu.

IGP Mangu alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Maafisa wakuu wa Polisi wakiwemo Makamanda wa Polisi wa mikoa, vikosi na makao makuu katika kikao kazi kilichokuwa kikifanyika jijini Dar es Salaam ambacho kilifunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi.
Alisema waendesha bodaboda wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za usalama barabarani lakini sasa mwisho wao umefika na kuwataka makamanda wa polisi wa mikoa kote nchini kutekeleza maelekezo hayo ili kuleta nidhamu kwa bodaboda katika kufuata sheria za usalama barabarani.
IGP Mangu alisema suala la kufuata sheria za usalama barabarani kwa bodaboda halina mjadala na kila kamanda ahakikishe kuwa wale wote wasiofuata sheria na kukaidi wanakamatwa bila kuoneana muhali kwakuwa wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuzuilika.
“ Pamoja na kuendelea kudhibiti uhalifu wa aina zote, natoa maelekezo  kwa kila mkoa kuhakikisha  unaendesha oparesheni kali  dhidi ya bodaboda ili kupunguza ajali zinazosababishwa na bodaboda ambao wengi wao hawataki kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani, tusiwaonee muhali maana maisha ya watu ni muhimu sana na jambo la msingi ni kusimamia sheria tu” Alisema IGP Mangu. 
Awali akifungua kikao kazi hicho Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Charles Kitwanga alilitaka Jeshi la Polisi kuendelea na mapambano yake dhidi ya uhalifu na wahalifu ili usalama wa raia na mali zao uendelee kuimarika na watanzania waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo bila hofu ya kutendewa uhalifu.  
Pamoja na agizo hilo la IGP Mangu,mwezi uliopita,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari akizungumza na na alisema kuwa Oparesheni hili ilikwishaanza kuanzia mwanzoni mwa mwezi Januari na mafanikio kadhaa yaliyojitokeza katika opaereheni hiyo ni pamoja na kukamata silaha kadhaa kutoka kwa wanamiliki silaha kinyume na sheria.
Asante kwa kuendelea kuchagu P5 TANZANIA MEDIA,Mshirikishe na mwenzio

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA