KIKAO CHA WATALAAMU,WATENDAJI NA WAKUU WA IDARA MBALIMBALI MANISPAA YA MPANDA KUFANYIKA KESHO.


Na.Issack Gerald-Mpanda
Kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Mpanda kinatarajia kufanyika kesho.

Kwa mjibu wa taarifa ya Afisa habari wa Manispaa ya Mpanda kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda,Bw.Pius Donald amesema kuwa,kikao hicho kinatarajia kufanyika katika ukumbi wa idara ya maji kuanzia majira ya Asubuhi.
Kikao hicho kitakachowashirikisha waandishi wa habari,pia kinatarajia kuwahusisha watalaamu mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda,wakuu na watendaji wa idara mbalimbali katika Manispaa ya Mpanda.
Kikao hiki kinafanyika ikiwa ni siku chache baada ya vikao vya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kufanyika karibu Halmashauri zote tano za Mkoa wa Katavi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA