JIPU KUBWA MPANDA KATAVI LATUMBULIWA,WATUMISHI 16 NJE,TUME KUANZA KAZI YAKE WATAKAOBAINIKA SHERIA ZANOLEWA YUMO NA MWANASHERIA WA MANISPAA YA MPANDA.


Na.Issack Gerald-Mpanda
BALAZA la Madiwani Katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,limewasimamisha kazi watumishi 16 wa Manispaa hiyo kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utumiaji ovyo wa fedha za manunuzi ya gari la kuzoa taka pamoja na ubadhilifu wa fedha ya skimu ya umwagiliaji maji ya kakese.

Watumishi hao 16,wamesimamishwa kazi kupitia kikao cha dharula ambacho kimefanyika jana Februari 26 katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Akitangaza majina ya waliosimamishwa kazi,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Philip Mbogo,amewataja kuwa ni  Bw.Chamilius Luhinda mwanasheria wa Manispaa,Vumilia Kakulima mkuu wa kitengo cha Manunuzi,Charles Ngonyani mkuu wa idara ya ushirika,chakula na umwagiliaji,Brian Severe mkuu wa idara ya ardhi mipango miji na maliasili,Vicent Kayombo mkuu wa idara ya elimu Shule ya Msingi,Abrahamu Kaswa afisa mipango miji,Bosko Kapinga mweka hazina wa Manispaa,Kibi Hamis Musaka Mhasibu Mwandamizi,Paschal Kweya afisa afya Mazingira Manispaa ya Mpanda,Gerigori Lugarema afisa maendeleo ya jamii msaidizi,Gorge Ngongolowo mhasibu mwandamizi,Albert Kiando mhandisi wa ujenzi,Victa Lutajumula mwalimu Mkuu daraja la pili,Focus Bilamule mhasibu Manispaa ya Mpanda,Jefu Julious  mhandisi umwagiliaji Manispaa na Said Madua Afisa mazingira wa Manispaa ya Mpanda.
Mh.Mbogo amewataja wanaokaimu nafasi hizo kuwa ni pamoja na Said Mohamed Hemed mkuu wa idara ya ushirika,chakula na umwagiliaji,Rashid Pili Idara ya elimu Msingi,Mabokera Mwakabamba kitengo cha Manunuzi,Paschal Sindani idara ya ujenzi,Juma Luhomwa mweka hazina wa Manispaa huku  Peter Charles Mkalipa atakaimu mkuu wa idara,ardhi na maliasili.
Hata hivyo Mh.Mbogo amesema kuwa nafasi ambazo hawajapatikana watakaokaimu nafasi zao kwa sasa utaratibu unaendelea ili kutokwamisha shghuli za Manispaa.
Kutokana na kusimamishwa kwa watumishi hao,balaza la madiwani limetaka kuundwa tume ya kuchunguza tuhuma hizo kwa ajili ya kuchulia hatua zaidi kwa wale watakaokuwa wamebainika zaidi.
Mwezi uliopita,Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Suleimani Lukanga alismamishwa kazi kwa tuhuma za kuhusika katika mamununuzi hewa ya gari ta kuzoa taka  na kutapanya pesa za umwagiliaji ambazo zilikuwa zaidi ya milioni 380 ambapo alisimamishwa na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI.
Endelea kuwa na P5 TANZANIA MEDIA.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA