CHENJI YA SHILINGI 500/=MKAZI SUMBAWANGA AHUKUMIWA MIAKA 10 KWA KUUA BILA KUKUSUDIA.


Na.Issack Gerald-Sumbawanga
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa imemhukumu kifungo cha miaka 10, mkazi wa kijiji cha Kazila Lizberth Fredinad (21) baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Charles Abel bila kukusudia.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Fredinad alimuua Charles Abel kwa kumchoma na kuni tumboni akigoma kumlipa marehermu chenji yake ya shilingi 500 aliyokuwa akidaiwa.
Akisoma hukumu hiyo jana, Jaji Mfawidhi Kakusulo Sambo alisema kuwa anatoa adhabu hiyo kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Awali Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali Happiness Mayunga alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 6, mwaka jana na kusababisha kifo.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa huyo aliingia katika kilabu cha pombe za kienyeji ambapo pia palikuwa panachomwa nyama ya nguruwe na kukuta wateja wengine wawili wakinywa pombe hiyo.
Ilielezwa kuwa ndipo marehemu alipoanza kumdai marehemu ampe chenji yake ya shilingi 500 na kusababisha ugomvi kuibuka baina yao na kuanza kupigana.
Kwa mujibu wa Wakili Mayunga ugomvi huo uliodumu kwa muda mrefu kila wakisuluhishwa waliendelea kupigana ndipo mstakiwa alipomchoma tumbo Charles kwa kuni na kumjeruhi vibaya ambapo alikimbizwa katika zahanati kijijini Kaengesa, Manispaa ya Sumbawanga kwa matibabu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA