AGIZO LA WAZIRI KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI BADO NDOTO,MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA KATAVI ATOA UFAFANUZI.


Na.Issack Gerald-Katavi
Agizo la naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi  Mh.Willium Tate Ole Nashe la kumtaka mrajisi vya vyama vya  ushirika hapa nchini kuteua  timu ya kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku wa Chama cha Ushirika Mpanda Kati wanaolalamika kutolipwa madai yao karibu milio 600 halijatekelezwa.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na  Mpanda Radio fm Ofisini kwake,Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Katavi Bw.Luhiguza Medadi Sesemukwa amesema kuwa,taarifa iliyopo kutoka kwa mrajisi  ngazi ya taifa aliyeagizwa kufanya ukaguzi  huo amesema timu hiyo imechelewa kufika kutekeleza agizo la waziri kutokana na ukosefu wa fedha.
Bw.Sesemukwa amesema kuwa,wajumbe wa timu kutoka tume ya maendeleo ya ushirika  iliyoundwa na mrajisi wa vyama vya ushirika nchini inatarajia kufika Mkoani Katavi wakati wowote kuanzia leo.
Hata hivyo shirika la wakaguzi wa vyama vya ushirika COWASCO kutoka Mkoani Tabora kwa sasa wapo Mkoani Katavi kuanzia Februari 14 mwaka huu na wanaendelea ukaguzi wa madai ya wakulima.
Amesema mara baada ya timu kutoka Dodoma ambako ndiko makao makuu yao yaliko,wataungana na timu timu iliyotoka Tabora kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi na uchunguzi wa kina.
Agizo la naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi  Mh.Willium Tate Ole Nashe la kumtaka mrajisi vya vyama vya  ushirika hapa nchini kuteua  timu ya kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku wa Chama cha Ushirika Mpanda Katavi wanaolalamika kupokonywa mamilioni hayo ya fedha,lilitolewa Januari 11,mwaka huu akitoka agizo la kuundwa na kutumwa timu ya ukaguzi ndani ya siku 14 kuanzia siku ya agizo kutolewa.
Katika hatua nyingine amewataka wakulima waliotoa hoja ya madai yao kutuo uthibitisho wa vielelezo ili kubaini ukweli wa malalamiko.
Mbali na malalamiko ya kutoripwa kitita hicho karibu miloni 600,pia walilalamikia  kulipwa kwa thamani ya dola badala ya shilingi,kuuziwa pembejeo kwa bei kubwa na kulipa kwa dola na kutokuona msaada wa Chama kikuu cha ushirika LATCU kwa wakulima wa zao la tumabku badal aya kuwanyonya.
Wakati huo huo,amewashauri Mrajisi Sesemukwa ametoa rai kwa wakulima kuendelea kupanda miti,kutumia Mabani ya kisasa ya kuchomea tumbaku yanayotumia kuni kidogo kwa ajili ya kuhifadhi mazingira.
Lakini pia amewataka wakulima kutotorosha tumbaku na kwenda kuuzia nje ya kampuni iliyoidhinishwa kununua tumbaku yake ili kuepuka kusababisha mlundikano wa madeni watakayodaiwa.
Majibu ya mrajisi wa Mkoa,yanakuja kufuatia malalamiko ya wakulima kuanza kujitokeza wakilalamika kutokuona agizo la waziri kutotekelezeka.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA