HIVI KUMBE HALI YA BEI YA DAGAA SUMBAWANGA RUKWA IKO HIVI?


Na.Issack Gerald-Sumbawanga
DAGAA maarufu kama kauzu wanauzwa kwa bei ya juu katika masoko ya mjini Sumbawanga mkoani Rukwa baada ya kuadimika katika kipindi hiki cha masika.
                                            
Miongoni mwa dagaa wanaouzwa Sumbawanga Mjini Kutoka Rukwa wakivuliwa kutoka Ziwa Tanganyika (PICHA NA.Issack Gerald)


Kitoweo hiki ambacho pia ni maarufu kama ‘dagaa wa Kigoma’ huvuliwa katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika katika wilaya za Kalambo na Nkasi mkoani Rukwa.
Imeelezwa kuwa kilo ya dagaa kwa sasa inauzwa kwa Sh 20,000 kutoka Sh 8,000 miezi mitatu iliyopita, ikiwa ni bei ya rejareja baada ya kuadimika sokoni katika Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa kwa miezi mitatu mfululizo.
“Msimu wa mvua dagaa hawa wanaadimika sana,isitoshe bidhaa hii ilikuwa imeadimika kabisa sokoni ambapo sasa bado wanavuliwa kwa taabu sana huku mahitaji ya walaji wakiwa makubwa,” alisema mchuuzi wa samaki aitwaye Samweli Kapele.
 “Lakini sasa mambo yamebadilika bei ya dagaa imepaa sana hata tunashindwa kuwatumia ndugu zetu waishio nje ya mkoa huu kama zawadi kwani kutokana na kipato cha baadhi yetu tunashindwa kuwanunua,”mmoja wa mkazi wa mjini Sumbawanga aitwaye, Mariam Kinsukulu alisema. 
Chanzo : Wafanyabiashara kutoka Rukwa hadi Katavi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA