HALI YA USALAMA BURUNDI HUENDA IKACHUKUA SURA MPYA


Na.Issack Gerald-Katavi
Hali ya kisiasa nchini Burundi huenda ikachukua sura mpya baada ya serikali na upinzani kutoafikiana juu ya yatakayozungumzwa kwenye mkutano ili kutatua mzozo nchini humo.
                                                    
Jaji Augustine Mahiga Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimatifa akiwa ni miongoni mwa viongozi wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki wanaoshuruhisha mgogoro wa kisiasa nchini Burundi

Kwa mujibu wa msemaji wa CNARED Jeremie Minani amesema kuona serikali ilikataa kuhudhulia mkutano ambao ungefanyika Januari 6,2016 jijini Arusha kuwa hawakuafikiana juu ya taerehe hiyo ilikuwa ni kisingizio.
Amesema wanapaswa kujadiliana juu ya mzozo wa Burundi ili wasije kutumbukia kwenye vita,kuachiwa huru kwa wafungwa dhidi ya maandamano,utumwaji wa wanajeshi wa AU na kuundwa kwa serikali ya mpito.
Kwa upande wa serikali,mshauri mkuu wa rais Willy Nyamitwe amesema kuwa mzungumzo yanatakiwa kujikita zaidi kwenye utatuzi wa mgogoro wa Burundi hasa utawala bora. Pia wanapaswa kushirikishwa warundi wato waliopo nchini na nje ya nchi.
Ingawa serikali ililalamika kuhusiana na kuhudhulia kwa wasiostahili kwenye mkutano uliofanyikia nchini Uganda Waziri wa ulinzi na usalama wa Uganda Crispus Kiyoga ameweka wazi kwamba pande zote zinapaswa kushiriki iwe ni serikali au upinzani bila kuegemea upande wowote.
Hata hivyo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Nkosazana Zuma ameitaka Burundi kukubali ujio wa wanajeshi hao wa kulinda usalama.
Itakumbukwa kuwa rais Pierre Nkurunziza ametishia kupigana na wanajeshi wa AU endapo watakanyaga ardhinim kwake bila ruhusa ya serikali ya Burindi.
Na. Bukuru Elias Daniel - Burundi

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA