SHULE BINAFSI MPANDA ZAOMBA RUZUKU KUENDESHA SHULE ZAO ILI KUTEKELEZA AGIZO LA SERIKALI


Na.Issack Gerald-MPANDA
WASIMAMIZI  wa shule binafsi wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa Kuzipatia ruzuku za Uendeshaji endapo agizo la ada elekezi lililotolewa na serikali litapitishwa.

Ombi hilo limetolewa leo na Mkuu wa shule ya Sekondari Istikama iliyoko Katika Manispaa ya Mpanda Bw,SADICK ABDALLAH wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA ofisini Kwake.
 Bw,Abdallah amesema shule binafsi hutumia gharama kubwa katika uendeshaji wake ikiwemo Kuwalipa Mishahara walimu, hivyo Kupunguzwa kwa Kiwango cha ada Kinacholipwa na wanafunzi kwa sasa huenda Kikasababisha kupungua kwa ubora wa elimu unaotolewa na shule hizo.
Aidha Bw,ABDALLAH ameowaomba wasimamizi wa sekta ya elimu Kuhakikisha wanatoa mwongozo wa Mabadiliko hayo Kabla ya mwaka wa Masomo wa 2016 ili kutoa nafasi kwao Kujiandaa kwa utekelezaji huo.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA