MTOTO ANAYEDAIWA KUUWAWA NA ASKARI KWA RISASI MLELE AZIKWA


Na.Issack Gerald-MPANDA
Wazazi wakazi wa kijiji cha Kamsisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi wamekubali kuuzika mwili wa mtoto wao Moshi Saleh (17) anayedaiwa kuuwawa kwa kupigwa risasi za moto na askari wa wanyama pori wa shirika la hifadhi za Taifa Tanapa Mkoani hapa.

Mwili wa marehemu huyo ulilazimika kuhifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa siku tano baada ya wazazi wa marehemu na wakiwa na wafugaji kukataa kuzika mwili huo mpaka wafahamu chanzo cha kifo cha mtoto wao.
Mara kadhaa wakazi Mkoani Katavi wamekuwa wakiwalalamikia askari wa hifadhi za Taifa za wanyama Tanapa  kuwafanyia ukatiri.
Hata hivyo waratibu wa haki za binadamu Mkoani Katavi wiki iliyopita katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu ,walisema vitendendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu havikubaliki Mkoani Katavi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA