WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI



Na.Issack Gerald-MPANDA
WATU Wawili wanaokabiliwa na mashtaka ya kukamatwa na nyara za serikali, wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpanda na  kusomewa mashtaka. 

Hakimu Mkazi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Bw. Adira Amworo, amewataja washtakiwa hao kuwa ni Jastin Bruno mkazi wa Tompolo na Philbert Leo Uliza mkazi wa Ikuba.
Watuhumiwa hao walikamatwa na polisi tarehe 17 mwezi huu katika Kitongoji cha Tompola Kijiji cha Usevya Kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi wakiwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi milioni 60,.
Kesi hiyo imeahirishwa na itasikilizwa tarehe 23 mwezi huu, na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA