VIJANA MPANDA WAELEZA WALIVYONUFAIKA NA MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA DUNIANI


 
Vijana katika kongamano Mjini Dodoma katika maadhimisho siku ya vijana Duniani

Na.Issack Gerald-MPANDA
Vijana katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda walioshiriki kongamano la wiki ya Vijana Oktoba 14 mwaka huu,wamesema kuwa walinufaika sana na mafunzo mbalimbali ambayo wanatarajia kuyatumia na kufanikiwa katika shughuli za kijasiliamali.

Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA baadhi ya vijana Mussa Jonasi Katuka na Hamis Abdul wamesema miongoni mwa masuala amabyo walijifunza ni pamoja na usindikaji wa bidhaa,ufungashaji wa bidhaa,namna ya kutafuta masoko ya bidhaa na umuhimu wa kuwa katika vikundi ili kupata mikopo ya kuendeleza shughuli zao.
Kwa upande wake Fadhiri Secha amabye ni Afisa vijana Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda amesema kuwa,Halmshauri imejipanga kuwasimamia vijana au makundi yaliyosajiliwa kisheria kwa ajili ya kuyapatia mikopo ya kuendeleza shuguli ambazo wamezibuni.
Aidha,vijana na vikundi vya ujasiliamali vimetakiwa kufuatilia habari mbalimbali kupitia vyombo vya habari  na mitandao kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kufanya kwa ajili ya kuondokana na umaskini.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ina Jumala ya vikundi 156 vya ujasiliamali ambapo kuanzia mwezi  Julai hadi Nvemba mwaka huu vikundi vya wajasiliamali vipatavyo 20 vimepatiwa mikopo ambapo chanzo cha fedha ya mkopo ni asilimia tano(5%) ambayo hutengwa kutokana na mapato ya ndani ya Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda.
Kutengwa kwa asailimia 5% kwa ajili ya mkopo ni agizo la serikali kuu ya Tanzania kwa Halmshauri zote hapa nchini.
Maadhimisho ya wiki ya vijana duniani yalifanyika Oktoba 14 mwaka huu huko mkoani Dodoma ambapo kama ilivyo kawaida hutanguliwa na kongamano linaloanza Oktoba 8 na shrehe hizi ziliambatana na kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA