MGOGORO WA WAFANYABIASAHARA WA MATUNDA SOKO LA MPANDA HOTEL WAMALIZIKA

Na.Issack Gerald-MPANDA
Wafanyabiasahara wa matunda katika soko la Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda,wamewapongeza viongozi wa Manispaa,madiwani , maafisa masoko na Bibi afya  kwa kuwaruhusu kuuza matunda yao katika eneo wanalolitaka baada ya kufanya usafi wa kuridhisha.

Hayo yamebainishwa na wafanyabiashara hao wakati wakizungumza na Mpanda Radio sokoni hapo.
Katika hatua nyingine wamesema kuwa,mgogoro wa wafanyabiashara hao uliokuwepo kati yao na Mwenyekiti wa Soko hilo Bw.Boniface Mganyasi wa kumtaka ajiudhuru umetatuliwa.
Novemba 17 mwaka huu,wafanyabiasahara hao wa matunda waligoma kuondoka katika soko hilo wakidai kuwa haaiwezekani kuondoka katika soko hilo kwa kuwa soko hilo wanalitegemea kuendesha maisha yao na kusomesha watoto.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA