UVAMIZI OFISI ZA CCM SUMBAWANGA RUKWA,SAMANI ZA MWENYEKITI VYATUPWA NJE

Na.Mwandisi wetu-SUMBAWANGA.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wanaosadikiwa kuwa ni wanachama wa chama cha Mapinduzi, juzi wameivamia ofisi ya chama hicho ya wilaya ya Sumbawanga mjini.

Wananchi hao walitoa samani zote zilizoko kwenye ofisi ya mwenyekiti wa wilaya hiyo na kuzitupa nje, kwa kumtuhumu kuwa ameongoza vikao vilivyokata jina la mbunge anayemaliza muhula wake Aeshi Hilal aliyeshinda kwenye kura za maoni.

Wakiongea kwa jaziba mbele ya ofisi hizo za CCM, Wilaya ya Sumbawanga katika  barabara ya sokoine mjini Sumbawanga, wamesema hata siku moja hawawezi kuvumilia vitendo vinavyofanywa na Mwenyekiti wa CCM, wa wilaya hiyo Bw, Selemani Kilindu kwa chuki binafsi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA