YASIKUPITE,MATUKIO WIKI HII KATAVI KATIKA SIASA,UCHUMI,MAKUNDI MAALUMU

SUALA LA SIASA
Na.Issack Gerald-Katavi
WAGOMBEA wa nafasi mbalimbali za uongozi Mkoani Katavi  wameaswa kuacha kutoa rushwa ili kujipatia ushindi katika uchaguzi ujao.

Hayo yamesemwa na baadhi ya viongozi wa dini mkoani hapa Jumatano wakati wakizungumza na P5 TANZANIA.
Miongoni mwa viongozi hao wa dini ni Askofu mkuu wa makanisa ya New haverst nchini askofu Laban Ndimubenye, amesema wagombea wanaotumia rushwa kuingia madarakani hawafai katika maadili ya nchi.
Naye Kaimu sheikh mkoani katavi  wananchi waliojiandikisha wanapaswa kuwa tayari kwenda kumchagua kiongozi wanayemtaka ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.  

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KATIKA SEKTA YA USALAMA BARABARANI
KIKOSI cha usalama barabarani mkoani Katavi kimewatadharisha madereva kuacha kutumia vilevi ambavyo ndiyo chanzo cha ajali.
Akizungumza na P5 TANZANIA katika mahojiano,mmoja wa wawakilishi kutoka kikosi cha usalama barabarani Pc Dotto Anderson amesema ulevi unaweza kuepukika bila shuruti.
PC Anderson ameongeza kusema kuwa ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na ulevi, mwendo kasi na uelewa mdogo wa sheria za usalama barabarani.
Aidha abiria katika vyombo vya usafiri na jamii kwa ujumla wameaswa kutoa taarifa pindi ukiukwaji wa sheria za barabarani unapofanywa.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
WAKULIMA ZAO LA TUMBAKU MPANDA WAENDELEA KUGUBIKWA NA UMASKINI
Na.Issack Gerald

WAKULIMA  wa zao la tumbaku mkoani Katavi  wameendelea  kubakia katika  umasikini licha ya vyama vya ushirika na serikali kudai kuwepo kwa mafanikio katika sekta ya kilimo.
Wakizungumza na P5 TANZANIA Alhamisi ya Wiki hii  baadhi ya wakulima wamekosoa  mwenendo wa masoko ya zao hilo kwa kusema kuwa hauwanufaishi kama wakulima licha ya kuzinduliwa kwa Masoko ya zao hilo hivi Karibuni.
Kutokana na Malalamiko hayo Mmoja wa wajumbe wa chama cha msingi Mpanda kati cha Majalila bwana Emmanuel Kanyuka amesema hali iliyopo sasa katika Masoko ya tumbaku ni tofauti na ilivyokuwa hapo awali licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima hao.
Mamlaka ya Vyama vya Ushirika Mkoani hapa zimekuwa zikilalamikiwa na wakulima kwa kuweka mbele maslahi yao badala ya Mkulima.
Source,Alinanuswe Edward,Editor Mark Ngumba.13/8/2015.

 >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
JAMII WILAYANI MLELE YASHAULIWA KUWASAIDIA WASIOJIWEZA.
Na.Issack Gerald
Jamii Mkoani Katavi imeshauriwa Kusaidiana na taasisi zisizo za Kiserikali kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kutoa Misaada ya Kijamii ili Kupunguza idadi ya Watoto wa mitaani.
Akizungumza na P5 TANZANIA Alhamisi ya wiki hii,Mkurugenzi wa shirika la usevya Development Society UDESO lenye makao makuu yake Wilayani Mlele Mkoani Katavi bwana Edeni Ezekiel Waimba.
amesema Jamii inatakiwa kuacha kuwa tegemezi kwa Serikali na Mashirika  binafsi kwa Kujiunga na Vikundi mbalimbali vya Kusaidia watu wa Makundi maalum wakiwemo watoto yatima.
Bw. Waimba amesema kuwa kwa  mwaka 2014/2015 Shirika la UDESO limetoa misaada mbalimbali kwa watoto takribani 1500.





Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA